Sunday, March 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mbunge wa zamani Munde afariki dunia, mazishi yafanyika kesho

by TNC
February 3, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mbunge wa Zamani wa Viti Maalumu Tabora, Munde Tambwe, Afariki Dunia

Tabora – Mbunge wa zamani wa viti maalumu (CCM), mkoa wa Tabora, Munde Tambwe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Munde ambaye amewahi Halmashauri Kuu (NEC) unasafirishwa leo kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoa wa Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumatano, Februari 4, 2026 katika Manispaa ya Tabora baada ya swala ya adhuhuri.

Munde amewahi kuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora kwa misimu mitatu mfululizo.

Jaha Kaducha, mmoja wa wanafamilia ya Munde amesema, "Tumeondokewa na mtu muhimu kwenye familia. Munde ni zaidi ya kiongozi, mzazi na mlezi, tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha yake."

Mkazi wa Tabora, Mwajuma Abasi, amesema Munde alikuwa kiongozi imara, mwenye mapenzi mema kwa watu wa Tabora, kwani mara kadhaa akiwa bungeni alikuwa akichangia hoja zinazogusa maisha ya wana Tabora moja kwa moja.

"Kwa Tabora sijui tutaweka wapi haya machozi, ila ni Mungu tu ameamua kuchukua mja wake. Tunamshukuru. Munde alitugusa hasa wanawake, akatuwezesha kupata mikopo na hata gesi tulipika vizuri," amesema.

Kwa upande wake, Maria Kambilo amesema maisha ya mwanasiasa huyo yalikuwa zawadi kwa watu wa Tabora kutokana na utendaji kazi wake bora uliotukuka.

"Wananchi waliona na walifaidika naye kupitia mapambano yake dhidi ya matatizo ya wananchi wake.

"Alikuwa na mapenzi kwa watu wa Tabora, yaani alikuwa anapenda nyumbani na hata aende wapi, anajua yeye ni mzaliwa na mkazi wa Tabora, na hata akiona fursa lazima anawahi Tabora. Anakula na wa nyumbani," amesema.

Maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu na waombolezaji wanaendelea kumtembelea familia ya marehemu kumfariji.

Tags: afarikiduniakeshomazishiMbungeMundeYafanyikaZamani
TNC

TNC

Next Post

Transport pioneer Mohamed Hood Said dies at 90

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company