Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Kesi ya wizi wa shilingi milioni 62 inayomkabili Laila itaendelea wiki ijayo

by TNC
January 17, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam – Mahakama ya Wilaya ya Temeke imepanga tarehe 23 Januari 2026 kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya wizi wa shilingi milioni 62.8, inayomkabili Laila Khatibu (42).

Khatibu ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya African Energy Ltd, anakabiliwa na kesi ya jinai namba 4085 ya mwaka 2025 yenye shtaka moja la wizi.

Kesi hiyo ilipangwa Ijumaa, Januari 16, 2026 kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji, lakini shahidi wa jamhuri ambaye alitakiwa kutoa ushahidi wake amepata msiba.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda, anayesikiliza kesi hiyo ameahirisha hadi Januari 23, 2026 itakapoendelea.

Wakili wa Serikali Shabani Shabani alidai kuwa shahidi wa upande wa mashtaka ambaye alitakiwa kuendelea kutoa ushahidi Said Seif, amepatwa na msiba na hivyo ameshindwa kufika mahakamani.

"Kwa hali hii, tuomba mahakama ipange tarehe nyingine ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa Jamhuri," alidai.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.

Katika kesi msingi, Laila anadaiwa kati ya Januari 2022 hadi Agosti 2023, katika kituo cha kujaza mafuta cha Kurasini Flour kilichopo Wilaya ya Temeke, aliiba fedha za mwajiri wake.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuiibia kampuni hiyo shilingi milioni 62.8, fedha ambazo zilifika kwake kutokana na nafasi yake ya ajira.

Tags: ijayoinayomkabiliitaendeleakesiLailaMilioniShilingiwikiWizi
TNC

TNC

Next Post

Watu sita washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya dereva wa pikipiki Ngosha, Tabora

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company