Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Serikali ya Venezuela yawaachia huru wanasiasa wa upinzani na waandishi

by TNC
January 9, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Venezuela Yawaachia Huru Viongozi wa Upinzani na Wanaharakati

VENEZUELA – Serikali ya Venezuela imewaachia huru viongozi mashuhuri wa upinzani waliokuwa wamefungwa, wanaharakisi na waandishi wa habari raia wa ndani na wa kigeni katika kile ambacho serikali ilieleza kuwa ni ishara ya kutafuta amani.

Hatua hiyo imefanyika jana Alhamisi Januari 8, 2026 ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Nicolás Maduro wa nchi hiyo akamatwe na majeshi ya Marekani na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za biashara ya dawa za kulevya.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amekuwa akiweka shinikizo kwa washirika wa Maduro ambao sasa wanaongoza nchi hiyo wakubali maono yake kuhusu mustakabali wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, alisema kuwa kuachiwa kwao kulifanyika kwa ombi la Marekani.

Katika taarifa zilizotolewa, Trump aliisifu serikali ya rais kaimu Delcy Rodríguez, akisema: "wamekuwa wazuri sana… Kila kitu tulichotaka, wametupatia."

Jorge Rodríguez, ndugu wa rais kaimu na mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Venezuela, amesema kuwa idadi kubwa ya watu ingeachiwa, lakini hadi usiku wa Alhamisi haikuwa wazi ni nani hasa au ni watu wangapi wangeachiwa.

Kwa muda mrefu, serikali ya Marekani na upinzani wa Venezuela wamekuwa wakitaka kuachiwa wanasiasa waliokamatwa, wakosoaji na wanachama wa asasi za kiraia. Hata hivyo Serikali ya Venezuela imesisitiza kuwa haishikilii wafungwa kwa sababu za kisiasa.

"Chukulieni hili kama ishara kutoka kwa serikali ya Venezuela, inayolenga kwa ujumla kutafuta amani," imetangaza serikali.

Viongozi Mashuhuri Walioachiwa

Miongoni mwa walioachiwa ni Biagio Pilieri, kiongozi wa upinzani aliyekuwa sehemu ya kampeni ya urais ya 2024 ya mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, María Corina Machado.

Pia ameachiwa Enrique Márquez, aliyewahi kuwa kiongozi wa mamlaka ya uchaguzi na mgombea katika uchaguzi wa urais wa 2024.

Taarifa zinaonyesha Márquez na Pilieri wakikumbatiana na wapendwa wao mitaani nje ya gereza.

Pia wamo raia watano wa Uhispania pamoja na wakili mashuhuri wa Venezuela na Uhispania na mwanaharakisi wa haki za binadamu Rocío San Miguel.

Maoni ya Vikundi vya Haki za Binadamu

Makundi ya haki za binadamu na wanasiasa wa upinzani wamesema wametiwa moyo na hatua hiyo, ingawa wanafikiri ni ishara ya kisiasa tu ya kuiridhisha serikali ya Trump, ambayo imeruhusu waaminifu wa Maduro kuendelea kubaki madarakani huku ikiiwekea nchi hiyo shinikizo kupitia vikwazo vikali.

Alfredo Romero, kiongozi wa Foro Penal, ameonyesha matumaini akieleza kuwa huo ni mwanzo wa kweli wa kuvunjwa kwa mfumo wa ukandamizaji nchini Venezuela.

Awali, iliripotiwa kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Venezuela wa mwaka 2024 serikali ya nchi hiyo iliendesha msako na kuwakamata watu mbalimbali zaidi ya 2,000 ikiwatuhumu kuwa walipanga kuhujumu utawala wa Maduro.

Tags: HuruSerikaliUpinzaniVenezuelaWaandishiwanasiasayawaachia
TNC

TNC

Next Post

PM promises protection for informal sector jobs

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company