Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Shirikisheni sekta binafsi kwenye utafiti kupata matokeo chanya

by TNC
January 8, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Rais Samia Ahimiza Ushirikiano wa Sekta Binafsi katika Tafiti za Bahari Zanzibar

Unguja – Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wahadhiri na watafiti katika Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zanzibar kushirikiana na sekta binafsi ili tafiti zinazofanyika ziwe na matokeo chanya kwa taifa na wananchi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo Alhamisi Januari 8, 2026 wakati akifungua majengo ya IMS Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi.

Ujenzi wa majengo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambao unatekelezwa na Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuleta mageuzi ya uchumi hususani katika maeneo ya sayansi za bahari. Majengo hayo yamegharimu shilingi bilioni 11.

Kutafuta Matokeo Chanya kwa Wananchi

"Niwahimize wahadhiri na watafiti katika taasisi hii kushirikiana na sekta binafsi ili tafiti zinazofanyika ziwe na matokeo chanya kwa maendeleo ya nchi na wananchi," amesema Rais.

Pia, ameitaka taasisi hiyo kuanzisha mafunzo mafupi ya vitendo kwa wananchi wanaozunguka katika eneo hilo ambako wengi wanajishughulisha na masuala ya uvuvi, ili kuwaongezea tija na vipato katika kukuza uchumi wa buluu.

Amesema taasisi hiyo ni ya kimkakati Zanzibar kwani imebeba mustakabali wa wananchi na imeendelea kuwa nguzo muhimu katika uchumi wa bahari.

Wito kwa Wanafunzi

Katika hatua nyingine amewataka wanafunzi wanaosoma na watakaosoma katika taasisi hiyo, watumie fursa hizo kwa kufanya tafiti na bunifu katika matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.

"Mtakayoyafanya msiache kuwa waangalifu, ili kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunzwa na kuendelezwa," amesema kiongozi huyo wa taifa.

Kwa mujibu wa Rais Samia, tafiti katika uchumi wa buluu ni nguzo muhimu katika kukuza pato la taifa na kupanua ajira kwa taifa huku akibainisha kuwa tafiti zitasaidia katika kukuza sera za nchi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mapinduzi na Sayansi

Akizungumza kuhusu mapinduzi, Rais Samia amesema hayawezi bila kuwa na uwekezaji katika sayansi na teknolojia kwani ndio msingi katika bunifu na maendeleo ya kweli.

"Majengo haya yanaendana na tafsiri na malengo ya mapinduzi, kwahiyo kukamilika kwake haruka ni matokeo ya uwajibikaji, nidhamu, na uongozi unaoleta matokeo," amesema Samia.

Ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa ataendelea kuwekeza katika elimu ya juu katika kujenga uchumi shirikishi, shindani na endelevu.

Ametumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia kutoa mchango wake katika kujenga sekta ya elimu kutokana na fedha wanazotoa.

Maendeleo ya Chuo

Rais mstaafu ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho, Jakaya Kikwete amesema lengo la kuwekeza katika elimu limeendelea kupewa kipaumbele kwa kutekeleza miradi yenye matokeo ya moja kwa moja katika nchi.

Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya kujifunza na kufundishia na pia kinatekeleza tafiti mbalimbali.

Amesema kampasi za Kagera na Lindi nazo zipo katika hatua nzuri na ifikapo Oktoba mwaka huu kampasi hizo zitaanza kudahili wanafunzi.

Kwa mujibu wake, programu ya HEET imeendelea kukifanya UDSM kuwa kinara katika utoaji wa wataalamu katika sekta mbalimbali za kitaalamu.

Mahitaji ya Ziada

Hata hivyo, ametumia fursa hiyo kuomba mambo matatu iwapo wakipata awamu ya pili ya mradi huo au hata isipokuwepo basi Serikali iangalie namna ya kuwasaidia kupitia fedha za serikali.

Ameyataja mambo hayo ni pamoja na kumalizia bweni la wasichana, kuwajengea bweni la wavulana na kuwapatia chombo cha usafiri wa baharini kwa ajili ya kujifunzia.

"Kutokuwa na chombo hicho kunaleta upungufu mkubwa, tunaomba kama mradi huu wa HEET awamu ya pili haya tusaidiwe lakini hata kama hautakuwepo tunaomba serikali iangalie namna inavyoweza kutusaidia," amesema.

Ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuwezesha mambo mawili; hati ya eneo hilo na ujenzi wa barabara inayokwenda katika chuo hicho.

Miradi ya Taifa

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda amesema kupitia mradi huo kuna majengo mbalimbali kama hayo yanaendelea katika kampasi za chuo hicho kwa mikoa 16 nchi nzima ambapo kuna jumla ya majengo 1,177.

Profesa Mkenda amesema katika kuendeleza elimu kuna majengo yanagharimu dola za Marekani milioni 20 lakini mengine sio ya mradi wa HEET.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, amesema baada ya kukamilika mradi huo kutaleta manufaa makubwa kwa wanataaluma kubadilishana uzoefu na kutakuwa na fursa kupokea wataalamu bobezi.

Pia itaimarika kwa tafiti hususani uchumi wa buluu na kutoa suluhisho za changamoto na ubora wa ufundishaji na ufunzaji.

"Kukamilika kwa mradi huu ni hatua mpya ya maendeleo ambapo kutafungua programu mpya sita za bahari ikiwemo shahada ya uvuvi na teknolojia ya bahari na shahada ya ufugaji wa viumbe majini," amesema Profesa Anangisye.

Uwekezaji wa Mradi

Utekelezaji huu unaenda sambamba na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), unaotekelezwa na Serikali kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, kwa lengo la kuboresha mitaala na mazingira ya elimu ya juu ili yaendane na mahitaji ya soko la ajira.

Kupitia mradi huu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetengewa dola za Kimarekani milioni 49.5 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021 kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na jengo la taaluma na utawala na bweni la wanafunzi.

Tags: binafsichanyakupataKwenyematokeoSektaShirikisheniUtafiti
TNC

TNC

Next Post

Makonda, Katambi wapokea wizara, Simbachawene aondolewa

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company