Saturday, January 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Makonda, Katambi wapokea wizara, Simbachawene aondolewa

by TNC
January 8, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali, akifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, nafasi za Naibu Mawaziri pamoja na uongozi wa taasisi na uwakilishi wa kidiplomasia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 8, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka katika uteuzi huo, Patrobas Paschal Katambi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya George Simbachawene ambaye ametenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo, Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Rais Samia pia amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum). Profesa Kabudi kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika mabadiliko hayo, taarifa imesema Paul Makonda ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, nafasi ambayo awali alikuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo.

Aidha, Dennis Londo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, ambapo awali alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, huku Ayoub Mohamed Mahmoud akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katika ngazi ya Katibu Mkuu, Rais Samia amemteua Dk Richard Muyungi kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Dk Muyungi anachukua nafasi ya Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kwa upande wa uteuzi wa mabalozi, Rais Samia amemteua Mhandisi Zena Said, Waziri Salum ambaye alikuwa katibu wa Rais pamoja na Meja Jenerali Mbaraka Mkeremy kuwa Balozi.

Mbali na hao, ameteuliwa Ally Samaje kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), akichukua nafasi ya Dk Mussa Budeba.

Pia, Rais amemtengua Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), Profesa Eliakimu Zahabu.

TNC imebaini kuwa uapisho wa viongozi wote walioteuliwa utafanyika Januari 13, 2026 katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, kuanzia saa 8.00 mchana.

Tags: AondolewaKatambiMakondaSimbachaweneWapokeaWizara
TNC

TNC

Next Post

Hizi hapa athari zinazowakabili wanaotunza fedha ndani

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company