Saturday, January 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Sintofahamu uendeshaji wa Serikali ya Venezuela, kiongozi akifikishwa kortini

by TNC
January 4, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Maduro Huenda Akafikishwa Mahakamani New York Kesho

New York – Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, huenda akafikishwa mahakamani jijini New York, Marekani, kesho Jumatatu, Januari 5, 2026, baada ya kukamatwa na mamlaka za Marekani katika shambulizi la kushtukiza alfajiri ya jana na kumsafirisha kwa ndege hadi nchini humo.

Maduro na mkewe, Cilia Flores, wanakabiliwa na mashtaka nchini Marekani ya kula njama ya ugaidi wa mihadarati, kula njama ya kuingiza dawa za kulevya (kokeini) nchini humo pamoja na makosa yanayohusiana na silaha.

Jana, Januari 3, 2026, katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Marekani "itaisimamia" Venezuela kwa muda usiojulikana na itatumia akiba yake ya mafuta.

Trump hajaondoa uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Marekani nchini Venezuela. Makamu wa Rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez, amesisitiza kuwa Venezuela italinda rasilimali zake kwa ajili ya wananchi wake.

Mahakama ya Juu ya Venezuela, jana, iliamuru Rodríguez achukue nafasi ya Rais wa mpito mara moja kufuatia Maduro kuwa kizuizini nchini Marekani.

Hatua Inayopingwa Kipande Mbalimbali

Hatua ya kushangaza ya Serikali ya Marekani kumuondoa madarakani na kumkamata kiongozi wa nchi ya kigeni imepokelewa kwa pongezi kutoka kwa wafuasi wa Trump, lakini pia imekumbwa na ukosoaji kutoka pande zote mbili za kisiasa.

Baadhi ya wabunge wa Marekani wanahoji uhalali wa shambulio hilo na kueleza hofu kuwa linaweza kuingiza Marekani katika vita vingine vya gharama kubwa na vya muda mrefu.

Trump amesifu kile alichokiita operesheni "iliyopangwa kwa ustadi" wa kijeshi iliyodaiwa kusababisha kukamatwa kwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, na mkewe, Cilia Flores, huku Serikali ya Venezuela ikitaka ithibitishiwe uhai wa viongozi hao na kulaani hatua za Marekani.

Akizungumza saa chache baada ya kutangaza operesheni hiyo kupitia mtandao wake wa Truth Social mapema Jumamosi, Trump amesema operesheni hiyo ilihusisha mipango mizuri na vikosi bora vya kijeshi.

Mamlaka ya Urais Venezuela Yajikita

Wakati Mahakama ya Juu ya Venezuela ikiamuru Makamu wa Rais, Delcy Rodríguez, kuchukua madaraka ya urais kwa muda, Rais Trump ametangaza kuwa Marekani itaiongoza nchi hiyo kwa muda.

Operesheni ya kumkamata Maduro na mkewe wakiwa wamelala chumbani kwao ilifanywa na majeshi ya Marekani kwa kutumia zaidi ya helikopta za kijeshi 150 zilizovamia makazi ya Maduro.

Kufuatia kukamatwa kwa Maduro na kusafirishwa jijini New York kwa mashtaka, Venezuela imebaki bila Rais, na Mahakama ya Juu ilisema kuwa Makamu wa Rais Rodríguez lazima "achukue na kutekeleza mamlaka na majukumu yote ya urais kwa hadhi ya kaimu, ili kuhakikisha mwendelezo wa uendeshaji wa Serikali na ulinzi wa taifa kwa ujumla."

Katiba ya Venezuela inaeleza kuwa endapo Rais atashindwa kutekeleza majukumu yake kwa muda au kabisa, makamu wa rais ndiye anayepaswa kuchukua nafasi hiyo.

Hata hivyo, mahakama haikutangaza rasmi kuwa Rais Maduro hana uwezo wa kudumu wa kuendelea na majukumu yake.

Mahakama hiyo pia ilitangaza kuwa itaendelea kujadili suala hilo ili "kubaini mfumo wa kisheria unaopaswa kutumika kuhakikisha mwendelezo wa dola, uendeshaji wa serikali, na ulinzi wa mamlaka ya kitaifa, katika mazingira ambayo Rais hayupo kwa kulazimishwa."

Mvutano Kuhusu Uongozi

Wakati Mahakama ikitoa uamuzi huo, Trump naye katika mkutano na waandishi wa habari amesema kuwa Marekani itakuwa "ikiisimamia Venezuela kwa muda mfupi ili kuleta utulivu, hadi pale kutakapokuwa na uhamishaji wa madaraka kwa amani."

Trump amesisitiza kuwa hakutakuwa na uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Venezuela iwapo uongozi wa upande wa Venezuela "utazingatia matakwa ya Marekani."

Alipoulizwa iwapo wanajeshi wa Marekani watasaidia kuendesha nchi moja kwa moja, amejibu, "Hapana," akiongeza kuwa, "Iwapo Makamu wa Rais wa Maduro atafanya tunavyotaka, hakutakuwa na haja ya kufanya hivyo."

Amedai pia amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Makamu wa Rais Rodríguez na kwamba "anaelewa hali ilivyo."

Hata hivyo, Makamu wa Rais Rodríguez alitoa msimamo tofauti katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri, akisema, "Venezuela, kuna Rais mmoja tu, Maduro," na kusisitiza kuwa, "Rais Maduro ndiye kiongozi wetu na kamanda mkuu wa majeshi."

Hali hiyo imezua mvutano mkubwa wa kisiasa na kikatiba nchini Venezuela, huku jamii ya kimataifa ikiendelea kufuatilia kwa karibu mwelekeo wa uongozi na mustakabali wa nchi hiyo.

Tags: akifikishwaKiongozikortiniSerikaliSintofahamuUendeshajiVenezuela
TNC

TNC

Next Post

Wanaharakati washitushwa na ukamataji kuelekea uchaguzi

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company