Thursday, January 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Serikali yaonya ujazaji abiria kwenye vyombo vya baharini

by TNC
December 29, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Yawaonya Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri Baharini

Pemba – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeendelea kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri wa baharini kuepuka kubeba abiria kupita kiasi, huku wazazi na walezi wakitakiwa kupunguza idadi ya watoto wanaosafiri nao ili kuimarisha usalama wao safarini.

Wito huo umetolewa Desemba 29, 2025, na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ibrahim Saleh Juma, wakati wa ziara maalumu aliyofanya katika Bandari ya Mkoani, ambapo alibaini meli ya Silink 2 ikiwa imebeba abiria zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa.

Juma amesema kuwa katika kipindi hiki kuna ongezeko la abiria wanaosafiri kati ya Unguja, Tanga na Dar es Salaam, hali inayochangiwa na kufungwa kwa shule. Amesisitiza umuhimu wa vyombo vya usafiri kuzingatia idadi halali ya abiria ili kuepusha ajali na madhara yanayoweza kujitokeza.

Amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanapunguza idadi ya watoto wanaposafiri wakati wa mapumziko ya Desemba, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa usalama wao na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

"Tumefanya ziara ya kukagua eneo la usafiri kwenye Meli ya Silink 2 tumebaini ongezeko la abiria, kipindi hichi cha Desemba na Januari. Tukatoa angalizo kwa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanapakia abiria halali na sio kutumia kipindi hichi kwa kujaza abiria, kinyume na utaratibu waliowekewa kisheria," amesema.

Juma ameeleza kuwa meli inayoweza kuchukua abiria 1,500 mara nyingi inakutwa na watoto wasiopungua 400, hali ambayo inaweza kuleta shida. Vyombo vya usafiri vinapaswa kuwa makini katika kulinda usalama wa abiria wao.

"Vyombo vya usafiri vinapaswa kuchukua abiria kulingana na uwezo wa chombo. Kama ni abiria 1,500 wasizidishe, wahakikishe wanafuata mifumo ya ununuzi wa tiketi bila ya kuongeza idadi ya abiria kwenye vyombo vya usafiri," amesisitiza.

Ameongeza kuwa kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya abiria kipindi hiki, vyombo vya usafiri hutumia fursa hiyo kwa kuuza tiketi kwa bei ghali ambazo sio halali, jambo linalosababisha malalamiko kwa abiria.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Meli ya Silink 2, Saleh Suleiman Saleh, amesema wamekuwa wakijitahidi kufuata utaratibu kwa kupakia abiria wanaopaswa kulingana na uwezo wa meli. Hata hivyo, amedai changamoto kubwa inayojitokeza ni wazazi kusafirisha watoto wengi kwa wakati mmoja.

"Tumekuwa tukijitahidi kupakia abiria wanaotakiwa lakini changamoto inakuja baadhi ya wazazi wamekuwa wakisafirisha watoto wengi ambao hawalazimiki kukata tiketi. Mzazi mmoja anakuja na watoto sita na wote anataka akae nao kwenye viti, jambo hilo limekuwa likiwakwaza," ameeleza.

Amesema watoto wote wanaotaka kukaa kwenye viti baada ya kuingia kwenye boti, jambo ambalo limekuwa gumu, na kuomba wazazi na walezi kupunguza idadi ya watoto wakati wakisafiri.

Mratibu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kisiwani Pemba, Bakari Hamad Suleiman, amesema mamlaka hiyo imekuwa ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha utaratibu unafuatwa ili abiria wasafiri wakiwa salama.

Suleiman amesema ingawa kipindi hiki ni changamoto kutokana na ongezeko la abiria, hususan wanafunzi wanaosafiri kwenda masomoni na wengine kurudi nyumbani, mamlaka inajitahidi kuhakikisha kila safari inafanyika kwa njia salama na ya kisheria.

Tags: AbiriabahariniKwenyeSerikaliUjazajivyaVyomboyaonya
TNC

TNC

Next Post

Why people adopt foreign accents when living overseas

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company