Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Waziri azuru taasisi ya kidini, atambulisha jukumu jipya

by TNC
January 5, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Sangu Atembelea Makao Makuu ya Bakwata Dar es Salaam

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Uhusiano, Deus Sangu ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi wa Baraza hilo pamoja na kulitambulisha jukumu jipya la uhusiano ambalo Wizara yake imekabidhiwa kuratibu.

Sangu alipokelewa na Mufti na Mwenyekiti wa Bakwata, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, pamoja na wajumbe wa Baraza hilo, kala ya kufanya kikao cha pamoja cha kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa.

Akizungumza katika kikao hicho Jumamosi Januari 3, 2026, Waziri Sangu amepongeza kazi zinazofanywa na baraza hilo alizosema kuwa zina mchango mkubwa katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano nchini.

Amesema Bakwata limeendelea kuwa nguzo muhimu ya maadili na mshikamano wa kijamii kwa kuhimiza mazungumzo ya amani, kuvumiliana na uhusiano mzuri kati ya waumini wa dini ya Kiislam na nyingine.

"Juhudi hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kudumisha utulivu na mshikamano wa kitaifa," amesema Sangu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini katika kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa, pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, akitaja malezi bora na maadili kuwa msingi wa maendeleo ya jamii.

Pia, ameihakikishia Bakwata kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini, ikiwamo Bakwata, katika kuendeleza agenda ya amani, mshikamano na maendeleo jumuishi.

Awali akizungumza wakati anamkaribisha waziri huyo, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa masuala ya uhusiano na kuanzisha Wizara mahsusi inayosimamia eneo hilo.

Aidha, aliishukuru Serikali kwa kutambua na kuthamini mchango wa Bakwata, akiahidi kuwa Baraza hilo litaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na mshikamano nchini.

Tags: atambulishaazurujipyajukumukidiniTaasisiWaziri
TNC

TNC

Next Post

Uchaguzi mwingine mdogo kufanyika Kilimanjaro, Morogoro

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company