Friday, April 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Askari wapya waonywa dhidi ya siasa, kamari na madeni

by TNC
February 2, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Askari Wapya wa JWTZ Waonya Kuishi Kiapo cha Utii Msata

Msata, Pwani – Askari wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliohitimu mafunzo Msata mkoani Pwani, wametakiwa kukiishi kiapo cha utii wakati wote watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika sehemu mbalimbali watakazopangiwa.

Katika hilo, wameaswa kutotenda mambo ambayo ni kinyume na taratibu za kijeshi, ikiwemo kutojihusisha na siasa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matumizi ya dawa za kulevya, michezo ya kamari na kuepuka madeni yasiyo na tija.

Akizungumza wakati akifunga rasmi mafunzo ya askari hao wapya katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) Kihangaiko, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, amesema askari watakaokwenda kinyume na kiapo chao watachukuliwa hatua.

Amewataka askari hao kutunza afya zao na kuzingatia lishe bora wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Aidha, amewasisitiza wasijihusishe na uhalifu wa aina yoyote, kwani watakuwa wamekwenda kinyume na sheria na taratibu za kijeshi, hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Jenerali Mkunda amesisitiza askari hao kuwa tayari kiakili na kisaikolojia kuitetea nchi kwa kutekeleza majukumu ya Jeshi ndani na nje ya Tanzania.

Naye, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Kihangaiko, Brigedia Jenerali Sijaona Myala, amewapongeza askari hao waliohitimu mafunzo na kuwa tayari kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Brigedia Jenerali Myala amesema askari wapya wapo tayari kutekeleza majukumu mbalimbali ya kijeshi kutokana na mafunzo waliyoyapata.

"Shule ya RTS Kihangaiko itaendelea kushirikiana na makao makuu ya jeshi kuboresha mazingira ya mafunzo ili kuendelea kuwafunza vijana kuwa askari hodari watakaokuwa na uwezo wa kushiriki katika ulinzi ndani na nje ya nchi," amesema.

Tags: askariDhidikamarimadenisiasaWaonywaWapya
TNC

TNC

Next Post

How an American Revolutionary Built a Life of Service in Tanzania

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company