Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Sh4 bilioni kujenga kituo cha wasichana waathirika wa ukatili

by TNC
January 19, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kituo Kipya cha Nyumba Salama kwa Wasichana Waathirika wa Ukatili Kinajengwa Bagamoyo

Bagamoyo – Ukosefu wa nyumba salama kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia umeendelea kuwa chanzo kikubwa cha maumivu ya ziada kwa wasichana wanaokumbwa na vitendo hivyo nchini.

Badala ya kupata hifadhi ya muda, usalama na huduma za kisaikolojia baada ya kupitia ukatili, wasichana wengi hulazimika kurejea katika mazingira yaleyale yaliyowadhuru. Hali hii inaongeza hatari ya ukatili unaojirudia na kuathiri zaidi afya zao za mwili na akili.

Kukabiliana na changamoto hii, Shirika la Msichana Initiative limeanza ujenzi wa kituo maalumu ambacho kitakuwa nyumba salama kwa wasichana walioathirika na vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wakiendelea kupigania haki zao.

Kituo kinachojengwa Kiromo, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kitakuwa cha tano nchini. Bado kuna uhitaji mkubwa wa vituo vya aina hiyo kwa ajili ya kuwahifadhi waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia.

TNC imebaini kuwa harakati dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia zinakumbana na changamoto ya nyumba salama kwa waathirika, hali inayosababisha waendelee kupitia maumivu.

Mkurugenzi wa Msichana Initiative, Consolata Chikoti, amesema shirika hilo kupitia mkakati wake wa 2023-2027, ilibaini pengo la ukosefu wa makazi salama ya uhakika yanayozingatia mahitaji ya mtoto wa kike.

"Wasichana wanaonusurika katika ukatili, zaidi ya kuokolewa, wanahitaji matunzo, mwongozo, na muda wa kupona huku wakisaka haki," amesema Chikoti.

Ameongeza kuwa maelfu ya wasichana nchini Tanzania wanaishi katika hofu, ukatili, ndoa za utotoni, mimba za mapema na kunyimwa haki ya elimu na afya.

"Wasichana wengi wanapokimbia ukatili, hawana mahali salama pa kwenda. Mara nyingi wanarudishwa kwenye mazingira hatarishi kwa sababu hakuna nyumba salama za kutosha," alisema.

Baada ya kukamilika, kituo hicho kitatoa makazi ya muda kwa wasichana waliokumbwa na ukatili, msaada wa kisheria, huduma za kisaikolojia na shamba darasa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na ujuzi wa kujitegemea.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya shirika hilo lililoanzishwa mwaka 2016 kwa lengo la kutetea haki za wasichana, ikiwa ni pamoja kulinusuru kundi hilo na ndoa za utotoni.

Mwanzilishi wa shirika hilo, Rebeca Gyumi, amesema kuanza ujenzi wa kituo hicho ilikuwa ndoto ya muda mrefu katika kuunga mkono juhudi za kuwanasua wasichana katika mazingira hatarishi.

"Ujenzi huu unahitaji Sh4 bilioni. Wito wetu kwa wadau wengine na kila anayeguswa na haki za wasichana na wanawake achangie ili tulikamilishe hili na kituo kianze kufanya kazi," amesema Gyumi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Stella Msofe, amesema uwepo wa kituo hicho katika wilaya hiyo utaenda kuipunguzia mzigo Serikali hasa katika kipindi hiki ambacho matukio ya ukatili yameshika kasi.

"Bagamoyo matukio ya ukatili yapo na waathirika wapo. Kituo hiki kitakuwa msaada mkubwa kwa wilaya yetu," amesema Msofe.

Amewaomba wadau wengine na wote wanaoguswa katika suala hili kuchangia ili mawazo haya mazuri yaone utekelezaji wake kwa manufaa ya wasichana na jamii kwa ujumla.

Tags: BilionichakituoKujengaSh4UkatiliWaathirikaWasichana
TNC

TNC

Next Post

Vision 2050: Why the nation now sees investors as partners

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company