Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Rais Samia atoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mbunge

by TNC
January 18, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Rais Samia Atoa Rambirambi kwa Kifo cha Mbunge Halima Idd Nassor

Dar es Salaam – Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kifo cha Mbunge wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Halima Idd Nassor, aliyekuwa akiwakilisha kundi la wafanyakazi.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais kutoka Ikulu Januari 18, 2025, inaeleza kuwa Rais Samia amemtambua marehemu kama kiongozi mahiri aliyetoa mchango mkubwa kwa chama na Taifa, hasa katika kutetea maslahi ya wafanyakazi na kuchangia maendeleo ya jamii.

Rais ametoa pole kwa familia ya marehemu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), wanachama wa CCM, wabunge pamoja na jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

"Nawaombea wafiwa subira, faraja na nguvu katika kipindi hiki cha majonzi, huku tukimuomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina," ilieleza taarifa ya Ikulu.

UWT Wasema Kifo ni Pigo Kubwa

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, amesema kifo cha Halima ni hasara kubwa kwa jumuiya hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika chama na jamii.

"Tumeondokewa na mtu aliyekuwa anajituma sana katika utendaji wa kazi za chama na jumuiya. Alikuwa ni mtu tuliyekuwa tunamtumainia," amesema Chatanda.

Chatanda ambaye pia ni mbunge, amesema marehemu alihudhuria kikao cha kwanza cha Bunge baada ya kuahirishwa, lakini baadaye alianza kuugua kwa tatizo la moyo na kulazwa hospitalini.

"Jana nilienda kumuona hospitalini na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri, lakini asubuhi nimepigiwa simu nikaarifiwa amefariki dunia," alisema.

Historia ya Marehemu

Marehemu Halima alikuwa mtumishi wa umma katika idara ya ardhi kabla ya kugombea nafasi za uongozi ndani ya UWT kupitia kundi la wafanyakazi Tanzania Bara. Baada ya kushinda, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu.

Mbunge wa Kigamboni Aeleza Mshtuko

Mbunge wa Kigamboni, Allan Sanga, amesema kifo cha marehemu kimeacha mshtuko mkubwa kutokana na mipango na matarajio aliyokuwa nayo ya kuwahudumia wananchi wa Kigamboni.

Sanga alisema alikutana na marehemu kwa muda mfupi wakati wa kikao cha ufunguzi wa Bunge, ambapo marehemu alimahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi.

"Kifo chake kimenishtua kwa sababu alikuwa dada anayejua anachokitaka na alikuwa na malengo makubwa. Nilikuwa na matarajio ya kufanya kazi naye," amesema Sanga.

Marehemu alikuwa mkazi wa Kibada na wazazi wake wanaishi eneo hilo. Mazishi yatafanyika leo Jumapili, Januari 18, 2025 kwenye makaburi ya Kibada kwa Dole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Tags: atoachaKifokufuatiaMbungeRaisrambirambisalamuSamia
TNC

TNC

Next Post

Kufukuliwa mto kwarejesha tabasamu

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company