Tuesday, April 28, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Akutwa amefariki ndani ya gari Moshi, pombe kali yatajwa

by TNC
January 17, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kijana Afariki Ndani ya Nyumba Yake Moshi

Moshi – Kijana Deogratius James Ottaru (37), mkazi wa Kijiji cha Kilema Kati, Kata ya Kibosho Kirima, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake aliyokuwa akiishi peke yake.

Taarifa zinaeleza marehemu alifariki takribani siku mbili kabla ya kugundulika, hali iliyosababisha mwili wake kuvimba na kuanza kuoza, huku harufu kali ikiwashtua ndugu na majirani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza uchunguzi unaendelea.

"Askari walipofika eneo la tukio walibaini mlango wa chumba anachoishi ulikuwa umefungwa kwa ndani. Walipoingia walikuta mwili umelala chini na kulikuwa na harufu ya pombe," amesema Kamanda Maigwa.

Amesema kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda na majirani, marehemu alikuwa mtumiaji wa pombe kali na wakati mwingine alikunywa bila kula.

"Inawezekana ikawa ni sababu, lakini hiyo ni taarifa za awali. Mwili umechukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) kwa uchunguzi ambao utaonesha chanzo halisi cha kifo," amesema.

TNC imeshuhudia askari Polisi wakifika eneo la tukio Jumamosi Januari 16, 2026, wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Moshi, wakiambatana na madaktari kwa uchunguzi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidachini, Abuu Seleman Kwayi, amesema alipata taarifa za tukio hilo asubuhi kutoka kwa kamanda wa sungusungu.

"Nilipofika niliwauliza wanafamilia kama walishatoa taarifa polisi, wakasema tayari walishatuma ndugu kituoni na walikuwa wakisubiri askari wafike kwa ajili ya uchunguzi," amesema Kwayi.

Kwayi ametoa wito kwa vijana kuzingatia matumizi ya pombe na kuepuka kunywa kupita kiasi na kuishi kwa tahadhari.

"Unywaji wa pombe kupita kiasi si mzuri. Kuishi peke yako pia si salama. Kama angekuwa anaishi na mtu, huenda angepata msaada mapema," amesema.

Ndugu wa marehemu, Brightnes Ottaru amesema mara ya mwisho kuonana na Deogratius ilikuwa kipindi cha mwaka mpya lakini kwa hivi karibuni alishindwa baada ya juhudi za kuwasiliana naye kwa simu kugonga mwamba.

"Nilipigiwa simu asubuhi nikaambiwa ndugu yangu amefariki. Tulipofungua dirisha tukamwona ameanguka na amelala chini, tayari alikuwa ameshaanza kutoa harufu," amesema.

Brightnes anasema jirani mmoja alimwambia mara ya mwisho kumuona marehemu ilikuwa Alhamisi jioni, akieleza awali aliishi na mke wake kabla ya kutengana, huku mkewe akiishi kwao lakini akimtembelea mara kwa mara.

Kwa mujibu wa maelezo ya familia, mjomba wa marehemu ndiye aliyegundua tukio hilo baada ya kuona taa za nje zikiwa zimewaka asubuhi, akajaribu kugonga mlango bila majibu, kabla ya kuzunguka dirishani na kumuona marehemu akiwa amelala chini na kutoa taarifa Polisi.

Rafiki wa marehemu, John Kwayi, amesema kifo hicho kimewaacha wengi katika mshtuko.

"Marehemu ni mtu niliyesoma naye darasa moja na ni jirani wa karibu. Kifo chake kimenisikitisha sana, hadi sasa siamini kama amefariki," amesema.

Martina Joseph Mlayi, mke wa marehemu ambaye walikuwa wametengana tangu Julai mwaka jana, amesema kuna wakati marehemu alikuwa akilalamikia matatizo ya kiafya.

"Alikuwa akiniambia kuna nyakati anasikia kizunguzungu na anaanguka. Mara ya mwisho kumuona ilikuwa Alhamisi aliponitembelea nilipoishi Kwa Change," amesema.

Martina amesema marehemu ameacha watoto watatu, wa kwanza ana miaka 14 na anatarajiwa kuanza kidato cha kwanza, wa pili ana miaka mitatu na wa mwisho ana mwaka mmoja na nusu.

Tags: akutwaAmefarikiGarikaliMoshiNdanipombeyatajwa
TNC

TNC

Next Post

How youths disrupted burial of 18-year-old who died in police custody in Kilimanjaro

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company