Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Afariki dunia kwa kuangukiwa na jiwe kwenye machimbo

by TNC
January 16, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Msiba: Mchimbaji Mawe Afariki Baada ya Kudondokewa na Jiwe Pujini Pemba

Pemba – Juma Suleiman Juma (51) mkazi wa Pujini Kibaridi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki dunia baada ya kudondokewa na jiwe wakati akichimba mawe kwenye machimbo ya Makaani Pujini.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho walioshiriki shughuli ya kuuopoa mwili, wameeleza namna walivyopata taarifa za tukio hilo na kuanza harakati za uokozi.

Ali Suleimana Juma, kaka wa marehemu na mkazi wa Kijiji cha Pujini amesema muda mfupi walikuwa pamoja kwenye eneo hilo ingawa yeye alirejea nyumbani, lakini baadaye alipata taarifa za ndugu yake kuangukiwa na kifusi.

Amesema alipofika kwenye eneo la tukio na kushirikiana na wahisani wengine walianza kuutafuta mwili, walifanya juhudi ya kulivunja jiwe hilo ili kumtoa marehemu lakini walishindwa.

Harakati za Uokozi

Ridhiwani Asaa Abdalla mkazi wa Kibaridi Pujini amesema walipofika kwenye tukio waliona hali ni mbaya katika kuutafuta mwili wa marehemu huyo kutokana na kiambaza kizima cha jiwe kumuangukia.

Amesema walijitahidi kuvunja mawe juhudi hizo ziligonga mwamba na kuwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi kuja kushirikiana katika kuutafuta mwili wa kijana huyo.

"Kwa kweli nilipofika niliona hali ngumu jiwe kubwa lililomuangukia tukaanza kulikata lakini hata hivyo ilishindikana tukaamua kuwasiliana na wenzetu wa uokoaji kuja kusaidiana katika kuokoa mwili huo," amesema.

Suleiman Hilali Abdalla amesema walivunja jiwe hilo na kuona mwili, lakini hawakufanikiwa kuupata ndipo ilipokuja skaveta kusaidia katika uokoaji.

Ushirikiano wa Vikosi vya Uokozi

Kamanda wa Operesheni wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba, Mbarouk Ali Juma amesema wamepokea taarifa hizo na kufika eneo hilo kushirikiana na wananchi lakini kutokana na ukubwa wa jiwe walilazimika kuomba msaada kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya kupata skaveta.

"Tulipofika eneo ya tukio tuliwasiliana na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi kutuletea skaveta na walipokuja nalo tukaendelea na harakati za uokozi tukafanikiwa kuupata mwili lakini kwa taarifa za daktari alikuwa ameshafariki dunia," amesema.

Onyo kwa Wachimbaji Mawe

Akizungumza kufuatia tukio hilo Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame ametoa wito kwa wananchi hasa wanaofanya kazi ya uchimbaji wa mawe kufuata taratibu za kiusalama wakati wanapotekeleza majukumu yao.

"Niwaombe wananchi mchukue tahadhari wakati mnapofanya shughuli zenu hizi muangalie usalama wenu kwanza, tayari huyo ameshafariki na sisi tuwe makini katika kufanya harakati zenu," amefafanua.

Mkurugenzi huyo ametoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mwenzao.

Tukio kama hilo lilitokea Juni 29, 2024 katika Kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo watu wawili wa familia moja walipoteza maisha.

Tags: afarikiduniajiweKuangukiwakwaKwenyemachimbo
TNC

TNC

Next Post

Long-term reforms hinge on strong parliamentary oversight: Official

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company