Sunday, March 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Museveni ahitimisha kampeni, ahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura kesho

by TNC
January 14, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Uganda: Museveni Ahitimisha Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Kesho

Uganda – Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amehitimisha kampeni zake katika mkutano uliofanyika Kampala, huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho Alhamisi.

Mkutano wa kuhitimisha kampeni uliofanyika Jumanne Januari 13, 2026, ulishuhudia wananchi na wafuasi wa chama chake wakijitokeza kusikiliza sera za Chama cha National Resistance Movement (NRM) jijini Kampala.

Katika hotuba yake ya kufunga kampeni, Museveni amewahimiza wafuasi wake kupiga kura, akionya kuwa jaribio lolote la kuharibu uchaguzi litadhibitiwa.

Museveni Awania Muhula wa Saba Madarakani

Kiongozi huyo mwenye miaka 81 ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1986, na hivi sasa anawania muhula wa saba madarakani akichuana na mpinzani wake Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine anayegombea kupitia Chama cha National Unity Platform (NUP), anayeungwa mkono na vijana wengi nchini humo.

Akiwa mmoja wa marais wakongwe zaidi barani Afrika, serikali yake imebadilisha katiba mara mbili ili kuondoa vikwazo vya umri na idadi ya mihula, jambo lililomwezesha kugombea tena katika uchaguzi.

Hata hivyo, licha ya umri wake mkubwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu ukandamiziwaji wa wapinzani wa kisiasa, ukiukwaji wa haki za binadamu, na kashfa za ufisadi katika serikali yake, wafuasi wake bado wamesimama imara kumuunga mkono.

Wafuasi Wasema Kuhusu Uongozi wa Museveni

Mwanachama wa NRM, Emma Akello, amesema amefurahishwa na programu za vijana zilizoanzishwa na Museveni, lakini akaongeza kuwa fedha zaidi zinapaswa kuelekezwa kwa watu maskini zaidi.

"Rais amewekeza fedha nyingi kwa ajili ya vijana. Lakini watu walioko katika ofisi hizo wanapaswa kutafuta njia bora zaidi za kuhakikisha fedha hizo zinawafikia vijana, hasa vijana wa mitaani. Hawapati fedha hizo kwa sababu ya usimamizi mbaya," amesema.

Mfuasi mwingine wa NRM, Gloria Ninsiima, amesema kuwa chini ya uongozi wa Museveni, haki za wanawake zimezingatiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

"Tangu Museveni aingie madarakani, sisi wanawake tulioolewa. Zamani tulifungiwa jikoni, lakini sasa tunaweza kuzungumza hadharani," amesema.

Usalama Umeimarishwa Kuelekea Uchaguzi

Mamlaka za Uganda zimeanza kupeleka wanajeshi katika maeneo mbalimbali ya Kampala tangu Jumamosi, huku magari ya kulinda usalama yakisambazwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Kampala.

Tume ya Mawasiliano ya Uganda Jumanne imeagiza watoa huduma za intaneti ya simu kusitisha huduma kwa muda, ikitaja sababu za kusambaa taarifa za upotoshaji, udanganyifu wa uchaguzi na uchochezi wa vurugu.

Upinzani Unalalamika Ukandamizaji

Wapinzani wa Museveni katika kinyang’anyiro cha urais, akiwemo mwanasiasa mwenye umri wa miaka 43 na nyota wa muziki anayejulikana kama Bobi Wine, nao pia wamefanya mikutano ya kampeni.

Kiongozi huyo wa upinzani, aliyewahi kumpinga Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2021, amekuwa akifanya kampeni akiwa amevaa koti la kujikinga na risasi pamoja na kofia ya chuma ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya silaha za moto.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imesema kuwa uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya ukandamizaji na vitisho, huku mamlaka zikiwakamata mamia ya wafuasi wa upinzani.

Tags: ahimizaahitimishakampenikeshokujitokezaKupigaKuraMuseveniWananchi
TNC

TNC

Next Post

Rationing of electricity persists in Zanzibar despite new interventions

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company