Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Shinikizo kuachiwa wafungwa wa kisiasa 751 latua kwa kiongozi wa kanisa

by TNC
January 13, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Papa Leo wa Kumi na Nne Aombwa Kuingilia Kati Suala la Wafungwa wa Kisiasa Venezuela

Vatcan. Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, María Corina Machado, amezungumza na Papa Leo wa Kumi na Nne siku ya Vatican na kumuomba kuongeza shinikizo kuachiwa wafungwa wa kiasiasa takribani 751 wanaoshikiliwa na serikali ya Venezuela.

Machado amewaambia waandishi wa habari Januari 12, 2026 kuwa amemwomba Papa Leo aingilie kati ili kusaidia kuachiwa kwa mamia ya wafungwa wa kisiasa ambao bado wanazuiwa katika nchi hiyo iliyopo Amerika Kusini.

Papa Leo amesema kuwa anafuatilia kwa ukaribu yanayoendelea nchini Venezuela, na akatoa wito wa kulindwa kwa haki za binadamu na haki za kiraia katika nchi hiyo.

Nchini Venezuela, familia za watu waliokamatwa au kutoweka bado zilikuwa zikisubiri nje ya gereza ambako wapendwa wao wanashikiliwa.

Hadi kufikia Jumatatu alasiri, wafungwa wa kisiasa 49 pekee kati ya zaidi ya 800 walikuwa wameachiliwa huru, licha ya ahadi ya serikali kuachia idadi kubwa ya wafungwa hao.

Upinzani wa Venezuela kwa muda mrefu umekuwa na matumaini ya kumwondoa Rais Nicolás Maduro na kumweka madarakani mmoja wao ili kurejesha demokrasia nchini humo.

Hata hivyo, baada ya majeshi ya Marekani kumkamata Maduro na kumpeleka New York kukabiliwa na mashtaka ya biashara ya dawa za kulevya, Rais Trump alimruhusu naibu wake, Delcy Rodríguez, kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Tags: KanisaKiongoziKisiasakuachiwakwalatuaShinikizoWafungwa
TNC

TNC

Next Post

President highlights growth as island Revolution turns 62

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company