Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Madiwani wa Mufindi, Mafinga wanapewa mafunzo ili kuongeza ufanisi wao

by TNC
January 13, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Madiwani Mufindi na Mafinga Wapokea Mafunzo ya Uongozi Bora

Mufindi – Madiwani katika halmashauri za Wilaya ya Mufindi na Mji Mafinga wametakiwa kutumia vizuri mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo), kuimarisha uwajibikaji, ubunifu na ufanisi wa uongozi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Jumanne Januari 13, 2026, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi, Reuben Chongolo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Dk Linda Salekwa amesema kupitia mafunzo hayo, madiwani watapata uelewa mpana wa majukumu na mipaka ya madaraka yao kwenye usimamizi wa rasilimali za umma, mipango na bajeti kwenye halmashauri zao.

Chongolo amesema wananchi wanatarajia kuona matokeo chanya ya uongozi wao kupitia kutoa huduma bora katika maeneo yao, hivyo mafunzo hayo yatawaletea mabadiliko ya kiutendaji kutokana na kubadilika kwa nyakati.

"Niwasihi madiwani tujifunze kusikiliza ndipo tufanye uamuzi, badala yake tusiendelee na mazoea ya zamani mliyokuwa nayo kwa sababu nyakati zimebadilika, wananchi wanaangalia na wanatarajia kuona matokeo chanya," amesema Chongolo.

Kwa upande wake, mkufunzi kutoka Hombolo, Petro Nziku amesema mafunzo hayo ni elekezi kwa ajili ya madiwani, lengo likiwa kuwapa uelewa kuhusiana na majukumu na mipaka yao ya kiutendaji.

"Tumewapa nyenzo muhimu katika mada mbalimbali ikiwemo ya uongozi na utawala bora, sheria za serikali za mitaa, wajibu na stahiki zao kama madiwani, usimamizi wa fedha, mpango wa maendeleo na bajeti, maadili ya madiwani pamoja na kuwasimamia watumishi," amesema.

Pia, Nziku amewaasa madiwani kusikiliza kwa umakini kwa sababu Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya madiwani kupata mafunzo hayo.

"Mafunzo haya yatawawezesha kufanya kazi zao kwa tija, lengo kubwa ni kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi ili kutoa tabasamu kwa wananchi," amesema mkufunzi huyo.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Mufindi, Castory Masangula amesema mafunzo hayo yatawasaidia madiwani katika utekelezaji wa majukumu kwenye kata zao ukizingatia wengi wao ni wapya na hawajui namna ya utendaji kazi.

Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza kutolewa Januari 12, 2026 na yanatarajiwa kumalizika Januari 14.

Tags: ilikuongezaMadiwaniMafingamafunzoMufindiufanisiWanapewawao
TNC

TNC

Next Post

Mbunge Mbeya Vijijini kuvalia njuga kwa utunzaji wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company