Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watoto wawili wa familia moja waliopotea majini

by TNC
January 10, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Msiba: Watoto Wawili Wazama Kwenye Bwawa la Kuogelea Arusha

Arusha. Vilio na majonzi vimetanda katika familia ya Joachim Laizer, iliyopoteza watoto wawili kwa wakati mmoja, ambao wamekufa wakiogelea.

Abednego (13) na Ebenezer Joachim (9), walizama kwenye kina kirefu cha maji wakiogelea kwenye bwawa la kuogelea.

Tukio lilitokea Januari 7, 2026, ndani ya Hoteli ya Kilimanjaro Food, eneo la Sakina, jijini Arusha.

Taarifa za awali zinadai watoto hao walipelekwa hotelini hapo na mama yao kwa ajili ya kuogelea.

Mama yao aliwaacha kwa uongozi wa hoteli akaenda kufanya ununuzi wa mahitaji yao ya shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, amethibitisha tukio hilo Januari 9, 2026 akieleza uchunguzi bado unaendelea na taarifa rasmi kwa umma itatolewa.

"Ni kweli tukio limetokea, lakini uchunguzi bado unaendelea. Taarifa kamili itatolewa pindi uchunguzi utakapokamilika," amesema.

Baba Alalamika Kukosekana kwa Uangalizi

Akizungumza nyumbani kwake, Joachim Laizer, baba wa watoto hao amesema Abednego alikuwa amemaliza darasa la saba na alikuwa anatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, huku mdogo wake Ebenezer alitarajiwa kuanza darasa la nne.

Amesema anahisi kuna uzembe uliosababisha vifo vya watoto wake, akisisitiza ilipaswa kuwapo uangalizi wa mtu mzima wakati watoto wanapoogelea.

"Nikiwa namhudumia baba yangu Hospitali ya KCMC Moshi, nilipigiwa simu nikaelezwa kuwa watoto walizidiwa na maji walipokuwa wanaogelea na wamewahishwa Hospitali ya St. Joseph. Nilijiuliza inakuwaje watoto wanaogelea bila msimamizi? Nilishangaa sana," amesema.

Amesema ingawa watoto wake hawawezi kurejea, anataka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika ili iwe fundisho kwa maeneo mengine ya burudani.

"Natamani mwenye hoteli achukuliwe hatua, si kwa ajili yetu tu bali iwe funzo kwa wengine. Pia hoteli yenyewe ichukue hatua za kuhakikisha usalama wa watoto wengine kwa wakati mwingine," amesema.

Hoteli Inadai Ni Ajali

TNC ilifika hotelini hapo, ambako kiongozi ambaye hakujitambulisha jina zaidi ya kueleza ni meneja uendeshaji amesema tukio hilo ni kweli limetokea na hakuna uzembe, bali ni ajali kazini.

"Huo uzembe mnasema ninyi sisi hatuna taarifa za uzembe wowote kama mnataka taarifa zaidi nendeni Polisi wana taarifa zaidi za tukio," alisema Januari 8, 2026.

Hata hivyo, mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina, akiwanukuu wenzake, anadai wakati watoto hao wakiogelea mmoja alizama majini kwenye kina kirefu ambako watu wazima huogelea, hivyo mwenzake alijaribu kumuokoa, ndipo wote wawili wakazama.

"Kawaida watoto wakienda kuogelea kunakuwa na msimamizi ambaye hufuatilia mienendo yao, wasisogee penye kina kirefu lakini siku hiyo hakukuwa na mtu anayewafuatilia ndiyo maana wakakosa msaada wa haraka hadi mauti yakawakuta," amedai.

Jamii Nadai Uchunguzi wa Kina

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimnyaki, Samweli Meliyo, amesema tukio hilo limewashtua na kuwasikitisha.

"Kupoteza watoto wawili kwa mkupuo ni pigo kubwa kwa familia na jamii, tunaomba vyombo vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina kubaini kama kulikuwa na uzembe na iwapo utabainika, hatua za kisheria zichukuliwe," amesema.

Taarifa zinadai watu wanne wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo wakati uchunguzi ukiendelea.

Tags: familiamajiniMojawaliopoteaWatotoWawili
TNC

TNC

Next Post

Matokeo ya darasa la nne 2025 yametangazwa

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company