Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mtoto afa kwa kutumbukia shimoni

by TNC
January 9, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Tabora: Mtoto Afariki Baada ya Kutumbukia Shimoni Lenye Maji

Tabora – Mtoto wa miaka mitatu na nusu aitwaye Yasini Sadiki, mkazi wa Kitongoji cha Itetemia, Kata ya Itetemia Manispaa ya Tabora, amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji wakati akicheza na wenzake.

Shimo hilo linalodaiwa kumilikiwa na mchungaji mmoja Tabora Mjini ni maalumu kwa ajili ya kuchimbwa mchanga ambao hutumika kwa ujenzi.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Tabora, Loshpay Laizer baada ya kuopoa mwili wa mtoto huyo, amewahimiza wananchi kuwa makini na karibu zaidi na watoto wao hasa kipindi hiki cha mvua ambapo mashimo mengi yamejaa maji.

"Kipindi tulichonacho ni kizuri kwa ajili ya kilimo ili kupata chakula lakini ni kipindi hatari kwenye mazingira yetu hasa maeneo yenye mashimo kama haya ni hatari zaidi kwa watoto na hata watu wazima," amesema.

Ameshauri wamiliki wa mashimo ya biashara ya mchanga ili kutokua hatarishi kwa wananchi wengine hasa walio jirani na mashimo hayo kwani inakuwa kikwazo kwa michezo ya watoto na hata matumizi ya njia zilizo karibu na mashimo hayo.

"Ni kweli kwamba watu wanafanya biashara ya kuuza hii michanga lakini ni vyema kuwalinda na watumiaji wengine wa ardhi juu ya usalama wao," ameongeza Loshpay.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Itetemia lilipotokea tukio hilo, Joel Baruti amesema mtoto huyo akicheza na wenzake kando ya shimo hilo alikanyaga ukingoni kwa bahati mbaya akawa ametumbukia hapo ndipo wenzake wakaanza kupiga kelele wakikimbia kuelekea nyumbani kutoa taarifa.

"Kando ya shimo kuna kama njia ambayo watu hua wanapita na kipindi hiki cha mvua kingo za mashimo zinakatika na ndio kilichotokea kwa mtoto Yasini na wakati sasa kwa mmiliki wa shimo kuona namna bora ya kukinga shimo lake," amesema mwenyekiti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya majanga na furaha wa kata hiyo Idd Tambwe ameiomba serikali kuhakikisha inadhibiti mashimo yanayopelekea vifo vya watu katika kata hiyo kwa kuwachukulia hatua kali wamiliki wake kwa sababu ni muda mfupi sana tangu kufariki mtoto mwingine kifo cha aina kama hiyo.

"Serikali ichukue hatua kali kwa hawa watu wanaochimba mashimo na kuyaacha hovyo kwa sababu yana gharimu maisha ya watu na sio watoto tu na kwamba haina tija kutoa pole kwa wananchi kila mara halafu vifo vya aina hiyo vinajirudia kila siku," ameomba.

Hamisi Ramadhani mkazi wa Itetemia ambaye pia ni shuhuda wa tukio hilo amesema wakati wanapita njia akiwa na wenzake wakaona watoto wanapiga kelele wanakimbia ndio kusogea eneo hilo na kuona viatu vya mtoto vinaelea kwenye bwawa.

"Sisi tulivyoona kuwa ni mtoto amezama kwenye maji nikampa mwenzangu simu anishikie nikatumbukia kumuokoa mtoto lakini haikuwa bahati yetu maana alikuwa ameshafariki," amesema.

Tags: afakutumbukiakwamtotoshimoni
TNC

TNC

Next Post

Samia tasks marine scholars to drive blue economy agenda

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company