Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wazazi wakumbushwa kuwasimamia watoto kielimu

by TNC
January 8, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Unguja – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu Zanzibar, Dk Saada Mkuya Salum amesisitiza kuwa maendeleo ya elimu kwa mtoto sio jukumu la mwalimu pekee, na kuwa wazazi wanapaswa kuwasimamia watoto kila hatua ili kupata haki yao ya elimu.

Waziri huyo amesema ushirikiano baina ya wazazi na walimu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio ya watoto, na kuwa endapo wazazi na walezi watakuwa tayari kuwasimamia watoto wakiwa nyumbani, hakuna sababu ya kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Dk Saada amebainisha hayo leo Alhamisi Januari 7, 2026 katika hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Potoa ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Serikali imeshafanya jukumu lake la kutengeneza miundombinu ya skuli na vifaa, hivyo kilichobaki ni wazazi na walezi kuwasimamia watoto wafikie mafanikio ya elimu," amesema Waziri huyo.

Pia, Dk Saada amewataka wazazi kuhudhuria vikao vinavyoandaliwa na walimu skuli kwani vinatoa mustakabali wa wanafunzi, hivyo waache tabia ya kutohudhuria vikao hivyo.

Vilevile, amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kwani kabla ya Mapinduzi wazee walikosa haki yao ya elimu jambo ambalo lilisababisha umaskini wa maarifa.

Amesema Mapinduzi ya fikra ni matumaini ya kuleta mageuzi nchini kwenye sekta mbalimbali na kurahisisha utendaji kazi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Amos John amesema skuli hizo zimegharimu Sh6 bilioni.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Unguja, Rashid Simai Msaraka amesema uboreshaji wa sekta ya elimu ni kuifanya kuwa imara ili baadaye wayalinde Mapinduzi kwa kutumia elimu na sio kwa mapanga.

Ameeleza kuwa majengo hayo yanaendana na matokeo kwani ufaulu unaongezeka kwa kiasi kikubwa.

Tags: kielimukuwasimamiawakumbushwaWatotowazazi
TNC

TNC

Next Post

Highlighting Inclusive Trade for Sustainable Economic Growth

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company