Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Maduro kufikishwa mahakamani leo

by TNC
January 5, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Maduro Anatarajiwa Kufikishwa Mahakamani Marekani Leo

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Marekani leo baada ya kukamatwa mwishoni mwa wiki na vikosi vya Marekani, huku Rais wa Marekani, Donald Trump, akiweka wazi uwezekano wa uvamizi mwingine iwapo Marekani haitapata inachokitaka kutoka kwa kiongozi wa mpito wa nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumapili, Trump alisema anaweza kuamuru shambulio jingine endapo Venezuela haitashirikiana na jitihada za Marekani kufungua sekta ya mafuta ya nchi hiyo na kukomesha biashara ya dawa za kulevya.

Pia alitishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Colombia na Mexico, na kusema kuwa utawala wa kikomunisti wa Cuba "unaonekana kuwa tayari kuanguka wenyewe."

Balozi za Colombia na wa Mexico mjini Washington, zilipoombwa kutoa maoni, hazikutoa majibu mara moja kutokana na kauli ya Trump.

Kauli za Trump zilitolewa siku moja kabla ya Maduro kupangwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Shirikisho mjini New York leo.

Uvamizi wa Kijeshi Caracas

Maduro alikamatwa wakati wa uvamizi wa kijeshi uliofanyika Jumamosi mjini Caracas, tukio lililozua hofu kimataifa na kulizamisha taifa la Venezuela katika hali ya sintofahamu.

Maofisa wa serikali ya Trump wameeleza kukamatwa huko kama hatua ya utekelezaji wa sheria inayolenga kumwajibisha Maduro kwa mashtaka ya jinai yaliyofunguliwa mwaka 2020, yakimshutumu kwa kula njama ya ugaidi unaohusiana na dawa za kulevya.

Hata hivyo, Trump mwenyewe amesema kulikuwa na sababu nyingine pia, akieleza kuwa uvamizi huo ulichochewa kwa sehemu na ongezeko la wahamiaji kutoka Venezuela wanaoingia Marekani, pamoja na uamuzi wa nchi hiyo wa kutaifisha maslahi ya mafuta ya Marekani miongo kadhaa iliyopita.

Marekani Yataka Kurejesha Rasilimali za Mafuta

"Tunarejesha walichokiiba," alisema Trump jana akiwa akirejea Washington kutoka Florida. "Sisi ndio wenye mamlaka."

Trump alisema makampuni ya mafuta yatarejea Venezuela na kujenga upya sekta ya mafuta ya nchi hiyo. "Watatumia mabilioni ya dola, na watatoa mafuta ardhini," alisema.

Tags: kufikishwaleoMaduromahakamani
TNC

TNC

Next Post

Tanzania's exports rise 12.7pc on strong commodity prices and services growth

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company