Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Serikali kuwasilisha bungeni muswada wa usajili wa watoto wachanga

by TNC
January 3, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Serikali Yaandaa Muswada wa Usajili wa Watoto Wachanga

Kibaha – Serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni katika Bunge lijalo Muswada wa Sheria ya Usajili wa Watoto Wachanga, hatua itakayoiwezesha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuanza kuwasajili watoto tangu kuzaliwa.

Lengo la hatua hiyo ni kuweka msingi imara wa utambuzi wa wananchi mapema, kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii, na kuimarisha mifumo ya usalama wa taifa.

Akizungumza Jumamosi Januari 3, 2025, katika kikao cha 28 cha Baraza la Wafanyakazi wa NIDA kilichofanyika Kibaha, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema usajili wa watoto wachanga utasaidia mtoto kutambulika kisheria tangu mwanzo wa maisha yake na kuondoa changamoto zinazojitokeza wakati wa usajili wa watu wazima.

Amesema hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma za afya, elimu, bima na huduma nyingine za kijamii, na kutoa takwimu sahihi za wananchi ambazo zitasaidia Serikali kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ufanisi.

Kaji pia amewataka wananchi zaidi ya laki tatu ambao vitambulisho vyao vimeshatengenezwa kuvichukua ofisini kwa ngazi ya wilaya.

Amesisitiza kuwa ucheleweshaji wa kuchukua vitambulisho unapelekea hasara kwa Serikali na kupoteza fursa ya wananchi kutumia nyaraka hizo kupata huduma mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, amesisitiza umuhimu wa weledi, uaminifu na maadili ya utumishi wa umma kwa watumishi wa NIDA, huku akihimiza mshikamano na ushirikiano kati ya taasisi za Serikali ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Baadhi ya wakazi wa Pwani, akiwemo Swaumu Mfyome amesema NIDA inatakiwa kuongeza juhudi za kutoa elimu na matangazo kuhusu vitambulisho vilivyo tayari ili kuwahamasisha wananchi kuvichukua na kuvitumia, hatua itakayosaidia kuepusha hasara kwa Serikali.

Tags: bungeniKuwasilishaMuswadaSerikaliUsajiliwachangaWatoto
TNC

TNC

Next Post

Watu wanne wapoteza maisha kwa kuzama majini

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company