Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Gari la abiria lapata ajali Kilimanjaro, abiria wanusurika

by TNC
January 3, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Ajali ya Basi la Kidia One na Lori Kwasadala, Hai – Watu Wawili Wajeruhiwa

Moshi. Abiria kadhaa wamenusurika kifo baada ya basi la Kampuni ya Kidia One lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Nairobi nchini Kenya kugongana na lori lililokuwa likitoka Arusha kwenda Moshi katika eneo la Kwasadala, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Katika ajali hiyo, watu wawili wamejeruhiwa, akiwemo kondakta wa basi la Kidia One na abiria mmoja, ambao walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ilitokea jana asubuhi baada ya dereva wa lori kupoteza uelekeo na kuligonga basi hilo upande wa ubavuni.

TNC imebaini kuwa kwa sasa dereva wa lori hilo, Kamombi Habibu Omari, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kusababisha ajali hiyo.

"Januari 3, majira ya saa 11 alfajiri, kulitokea ajali ya kugongana kwa magari mawili eneo la Kwasadala, Wilaya ya Hai, na kusababisha majeruhi wawili pamoja na uharibifu wa magari," amesema Kamanda Maigwa.

Ameeleza kuwa lori lililokuwa likitoka Arusha kwenda Moshi lilihama upande wake wa barabara na kuligonga basi la Kidia One lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Nairobi nchini Kenya.

Kamanda Maigwa amewataja majeruhi kuwa ni Aisha Raymond (35), mfanyabiashara na mkazi wa Nairobi, aliyeumia paja la mguu wa kushoto, pamoja na kondakta wa basi hilo, Mussa Sumari (29), ambao wote wanapatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyeshindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, huku jitihada za kuondoa magari hayo barabarani zikiendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewataka madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Tags: AbiriaAjaliGariKilimanjarolapatawanusurika
TNC

TNC

Next Post

Dereva aliyefungwa nje ya nchi arejea nyumbani, asimulia

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company