Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

‘Pasiwedi’ yazua tuhuma za Thadei Kweka

by TNC
January 2, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mahakama Yaamuru Thadei Kweka Kutoa Nywila ya Simu kwa Uchunguzi wa Jinai

Moshi – Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetoa amri ikimwamuru Thadei Kweka, anayedaiwa kuwa raia wa Marekani, kutoa nywila (password) katika simu yake ili Polisi waendelee na uchunguzi wa tuhuma za jinai zinazomkabili.

Amri hiyo imetolewa Desemba 31, 2025, na Hakimu Mkuu Mkazi, Herieth Mhenga, alipotoa uamuzi wa maombi ya jinai namba 000030237 ya 2025, yaliyowasilishwa na Jamhuri ikiomba mahakama itoe amri hiyo kwa Kweka.

Maombi hayo yaliwasilishwa pamoja na kiapo cha Abichi Masanga, ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro, na yaliwasilishwa kwa hati ya dharura.

Kupitia kiapo hicho, Masanga anaeleza kuwa mtuhumiwa bado hajafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo ambazo ziko kwenye uchunguzi kupitia jalada MOS/IR/3713/2025.

Katika kiapo, anaeleza taarifa hizo alizichapa katika kundi la WhatsApp. Anaeleza upelelezi umebainisha kuwa taarifa hizo za uongo zipo katika makundi hayo ya WhatsApp na yalichapishwa na mjibu maombi (Kweka) kupitia simu yake ya kiganjani aina ya Samsung Galaxy S23 Ultra.

Anaeleza simu ya mjibu maombi ilikamatwa na maofisa wa Polisi, ambao wameshindwa kuzifikia taarifa zozote zilizomo katika simu hiyo kutokana na kukosa password ambayo mjibu maombi pekee ndiye anayo.

Maombi hayo ya upande mmoja yalisikilizwa na kutolewa uamuzi bila mjibu maombi, mawakili wake au ndugu kuwepo mahakamani.

Uamuzi wa Mahakama

Katika uamuzi wa mahakama, ambao umeibua mjadala katika mitandao ya kijamii, Hakimu Mhenga aliyakubali maombi ya Jamhuri.

Hakimu amesema katika usikilizwaji wa maombi hayo ya upande mmoja, Wakili wa Serikali, John Mgave, ndiye aliyewasilisha hoja kuishawishi mahakama.

Hakimu amesema mahakama, baada ya kupitia kwa makini mawasilisho ya Wakili Mgave na kiapo cha Masanga, amebaini kuwa hoja anayohitaji kuiamua ni kama kuna sababu za msingi kuruhusu maofisa upelelezi kufikia taarifa zilizomo katika simu hiyo kwa ajili ya uchunguzi.

Amesema chini ya kifungu cha 32 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao, mahakama imepewa mamlaka ya kutoa amri ya ufichuaji wa data au mfumo wa tarakilishi kama itaona kuna sababu za kuamini ni muhimu katika uchunguzi wa jinai.

"Muombaji ameeleza kwa uwazi kuwa simu hiyo ndiyo sehemu kuu ya uchunguzi na kwamba mjibu maombi amekataa kuruhusu simu hiyo ichunguzwe, hivyo kulazimisha uingiliaji wa mahakama ili kutenda haki," amesema na kuongeza:

"Mwombaji pia ameonesha uhusiano uliopo katika kifaa (simu) na tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo, na kwamba uchunguzi unaoendelea umekwama kutokana na mjibu maombi kukataa kutoa nywila katika simu hiyo."

Amesema: "Wakati mahakama inatambua haki ya faragha, haki hiyo si ya moja kwa moja na inaweza kuwa na mipaka ya kisheria kwa ajili ya maslahi ya usalama wa umma na uchunguzi wa makosa ya jinai. Sheria niliyoitaja inaipa mamlaka mahakama kuwasaidia maofisa upelelezi kuondokana na vikwazo vya kukusanya ushahidi."

Kutokana na msingi huo, hakimu amesema anakubali ombi la Jamhuri na kumwagiza mjibu maombi kuwaruhusu maofisa wa vyombo vya dola kuingia katika simu yake kwa lengo la kuchunguza tuhuma hizo za jinai.

Pia amemwamuru mjibu maombi kutoa nywila ya simu hiyo kwa maofisa wa Polisi, na kwamba data zitakazochukuliwa zitakuwa tu kwa ajili ya uchunguzi wa jinai unaoendelea katika jalada namba MOS/IR/3713/2025.

Malalamiko ya Ndugu

Wakati mahakama ikitoa amri hiyo, yapo malalamiko ambayo hayajathibitishwa kuwa Polisi wamekataa kumruhusu Kweka kusaini hati ya idhini kutoka Ubalozi wa Marekani ili ubalozi pia uhusike katika suala hilo.

Mbali na madai hayo, ndugu hao wanadai hawajaonana na Kweka wala wakili aliyemkodi kushughulikia suala hilo, wakidai jambo hilo linakiuka haki za mshukiwa kama zilivyoainishwa na CPA.

Elizabeth Kweka, dada wa Kweka anayeishi Marekani, anadai aliwasiliana na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kuuthibitishia kuwa Kweka ni raia wa Marekani, si Mtanzania.

Taarifa nyingine kutoka kwa wanaharakati zinadai ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unawajibika kusimamia suala hilo kwa kuwa ni raia wao.

Tags: KwekaPasiwediThadeituhumaYazua
TNC

TNC

Next Post

Matatizo ya moyo na damu yanavyosababisha vifo vya ghafla

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company