Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

TRC yasitisha safari za reli ya kasi Morogoro–Dodoma kwa muda, yataja sababu

by TNC
December 31, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

TRC Yasitisha Safari za Treni ya Kisasa Kati ya Morogoro na Dodoma

Dar es Salaam – Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusitisha kwa muda safari za treni ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Morogoro na Dodoma kuanzia leo Desemba 31, 2025, kufuatia uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, Desemba 31, 2025, na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Machibya Shiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mvua zimesababisha athari katika maeneo ya Kidete wilayani Kilosa mkoani Morogoro na Godegode wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, hali iliyolazimu shirika hilo kuchukua hatua ya kusimamisha safari hizo kwa ajili ya usalama wa abiria.

Kutokana na hali hiyo, TRC imesema kuwa kwa sasa safari zote za SGR zitahudumia njia ya Dar es Salaam–Morogoro na Morogoro–Dar es Salaam pekee hadi pale matengenezo yatakapokamilika na usalama kuthibitishwa.

"Tunawaomba abiria wetu kubadili ratiba za safari zao kulingana na mabadiliko haya ya muda," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Oktoba 23, 2025 TRC ilisitisha safari za SGR kwa muda baada ya treni ya Electric Multiple Unit (EMU) maarufu kama treni ya mchongoko iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma kupata ajali katika kituo cha Ruvu mkoani Pwani.

Hatua hiyo ilisababisha abiria wanaotumia usafiri huo kulazimika kusubiri kwa muda usiojulikana.

Desemba 28, 2025 TRC ililazimika kuongeza safari za treni ya SGR ili kuwahudumia abiria waliopata usumbufu uliojitokeza kutokana na mvua zilizonyesha na kuathiri miundombinu ya reli hiyo sambamba na ratiba ya SGR.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi, wakati huduma hizo zikiwa zimeathirika, baadhi ya abiria walishindwa kuanza safari zao kulingana na ratiba iliyopangwa.

Tags: kasikwaMorogoroDodomamudareliSababusafariTRCYasitishayataja
TNC

TNC

Next Post

Wanasiasa watoa mwelekeo mpya 2026

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company