Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mamlaka ya Tabora yakataza kutoa vibali vya ujenzi mabondeni

by TNC
December 31, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Tabora Mkuu wa Mkoa Apiga Marufuku Ujenzi Mabondeni

Tabora. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na Idara ya Mipango Miji kuhakikisha haitoi vibali vya ujenzi katika maeneo ya mabondeni.

Amesisitiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya ujenzi holela katika maeneo korofi, ikiwamo kubomoa majengo yasiyo na vibali pale itakapobidi.

Chacha ametoa maagizo hayo Jumatano Desemba 31, 2025 alipofanya ziara ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua, huku akisema wananchi wanaoishi mabondeni wanakumbwa na athari kubwa ikiwamo nyumba kujaa maji, kubomoka, watu kusombwa na maji na kuhatarisha maisha yao.

Ametaja baadhi ya maeneo hatarishi kuwa ni pamoja na linalozunguka Bwawa la Italia lililopo Kata ya Mapambano, Manispaa ya Tabora, ambalo limepasuka kutokana na mvua kubwa, pamoja na kata za Mwinyi na Malolo.

Amesema halmashauri inapaswa kutembelea maeneo yote chini ya mamlaka yake ili kuhakikisha matumizi sahihi ya ardhi yanafuatwa.

Amesema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya makazi yajengwe huku yale ya kilimo yaendelee kutumika kwa shughuli hizo.

"Meya na timu yako msikae ofisini tu. Piteni huko muangalie tatizo lilipo kwa sababu maeneo haya ambayo wananchi wamejenga yalipaswa kutumika kwa kilimo, labda mpunga. Tuchukue tahadhari mapema badala ya kusubiri kuokolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoazi," amesema Chacha.

Kwa upande wake, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulam Dewji amesema changamoto kubwa inayoikumba Idara ya Mipango Miji ni ujenzi holela, huku akieleza kuwa baadhi ya maeneo kama Malolo yanahitaji ujenzi imara wenye gharama kubwa.

Amesema halmashauri ina mpango wa kutoa notisi ya kuendelezwa kwa majengo imara na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo, watapaswa kuwauzia wenye uwezo wayaendeleze.

"Tunalitekeleza hili kwa kusimamia sheria. Naomba Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tabora iwe karibu nasi, kwa sababu utekelezaji wa sheria huwa na malalamiko na kelele za hapa na pale kuhusu nani yuko sahihi na nani amekiuka utaratibu," amesema Dewji.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) Wilaya ya Tabora, Subira Manyama amewashauri wananchi wanaojenga vidaraja binafsi kwa ajili ya biashara au makazi yao, kutumia wataalamu wa Tarura ili kujenga yanayokidhi vigezo.

Amesema ujenzi usiozingatia utaalamu unasababisha maji kushindwa kupita wakati wa mvua, hivyo kujaa na kuingia kwenye makazi ya watu jambo linaloleta madhara na kuhatarisha maisha.

"Sio kosa mtu kujenga daraja lake mwenyewe, lakini ni muhimu kutumia wataalamu kuepusha madhara wakati wa mvua kubwa kwa sababu maji hujaa haraka na kushindwa kupita," amesema Manyama.

Tags: kutoamabondeniMamlakaTaboraujenziVibalivyayakataza
TNC

TNC

Next Post

Plan pulls 0.4m families out of poverty trap

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company