Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Gaikwad kortini akidaiwa kujipatia Sh457 mil za mitambo ya Excavator

by TNC
December 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mfanyabiashara wa India Akabiliwa na Mashtaka ya Udanganyifu wa Sh457 Milioni

Dar es Salaam – Mfanyabiashara na raia wa India, Dharmendra Gaikwad (49) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kujipatia Sh457 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Gaikwad anadaiwa kujipatia fedha hizo kwa madai kuwa angemuuzia Hezron Kamali, Lorry aina ya Tipa na Excavator ambayo ni mitambo inayotumika katika ujenzi, migodini na bandarini.

Mbali na Gaikwad, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ni kampuni ya Al-Zahria Tanzania Limited.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani Jumanne, Desemba 30, 2025 na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na wakili wa Serikali, Titus Aron.

Wakili Aron amemsomea mshtakiwa huyo mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Kabla ya kumsomea mashtaka hayo, Hakimu Beda alimueleza mshtakiwa huyo kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Maelezo ya Mashtaka

Akimsomea mashtaka hayo, wakili Titus alidai shtaka la kwanza ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, tukio analodaiwa kulitenda Februari 28, 2025 eneo la Vingunguti, ambapo mshtakiwa alijipatia Sh82 milioni kutoka kwa Hezron Kamali, kwa madai kuwa atamununulia excavator, wakati akijua sio kweli.

Februari 14, 2025 mshtakiwa huyo alijipatia Sh40 milioni kutoka kwa Kamali kwa madai kuwa atamuuzia excavator.

Shtaka la tatu, Julai 2, 2025 eneo la Vingunguti kwa lengo la kudanganya, mshtakiwa alijipatia Sh200 milioni kutoka kwa Kamali, kwa madai kuwa atamuuzia excavator, wakati akijua sio kweli.

Tarehe hiyo pia mshtakiwa alijipatia Sh73 milioni kutoka kwa Kamali kwa madai kuwa atamuuzia Tipa, wakati akijua kuwa ni uongo.

Vile vile, mshtakiwa huyo pamoja na kampuni hiyo, walijipatia Sh62 milioni kutoka kwa mlalamikaji kwa madai kuwa wangemuuzia mtambo wa excavator.

Shtaka la sita ni kutakatisha fedha, ambapo kati ya Machi 28 na Julai 2, 2025 eneo la Vingunguti lililopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa alijipatia jumla ya Sh457 milioni kupitia akaunti benki ya Absa yenye jina la Al-Zahria Tanzania Limited, wakati akijua ni mazalia ya kosa tangulizi la kujipatia pesa kwa udanganyifu.

Uamuzi wa Mahakama

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haijakamilika hivyo wanaomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Nyaki aliahirisha kesi hadi Januari 8, 2026 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Tags: AkidaiwaExcavatorGaikwadkortinikujipatiamilMitamboSh457
TNC

TNC

Next Post

Tanzania yavuna Sh26.95 trilioni kwenye uwekezaji, nchi moja ya Asia kinara

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company