Thursday, January 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

CCM yashinda ubunge Fuoni

by TNC
December 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

CCM Washinda Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Fuoni Zanzibar

Unguja. Chama Cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo wa mbunge Fuoni Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo usiku wa Desemba 30, 2025 katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Wilaya ya Magharibi B, Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo, Miraji Mwadini Haji amemtangaza Asha Hussein Saleh kuibuka mshindi.

Katika matokeo hayo, Asha amepata kura 9,861 akifuatiwa na mgombea wa ACT Wazalendo, Khamis Shaib Mussa ambaye amepata kura 503 ya kura zote zilizopigwa.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo, waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 14,130, waliopiga kura ni 11,024, kura halali 10,930 na zilizoharibika ni 94.

"Kwa mantiki hiyo namtangaza Asha Hussein Saleh wa CCM kuwa mshindi wa jimbo la Fuoni," amesema Miraji.

Licha ya ACT kupata nafasi ya pili, lakini chama hicho kimesema hakikushiriki katika uchaguzi huo badala yake Tume imetumia mgombea yuleyule aliyekuwa katika orodha ya wagombea waliokuwapo katika orodha ya uchaguzi mkuu, kabla ya kuahirishwa.

Uchaguzi wa mbunge wa Fuoni umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Ali Mwinyi ambaye ni kaka yake mkubwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Kifo cha Abbas Mwinyi kilitokea Septemba 25, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Lumumba, Zanzibar.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Asha amewashukuru wananchi waliompigia kura akiahidi kushirikiana nao kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.

"Nawashukuru wananchi wa Fuoni kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi niwe mbunge wao, ninachowaomba tena ni kunipa ushirikiano ili tukaijenge Fuoni kwa maendeleo," amesema Asha.

Baadhi ya waliokuwa wagombea kupitia vyama vya DP na CUF, wamesema wapo tayari kushirikiana na aliyeshinda kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo.

"Uchaguzi umeisha aliyeshinda kashinda, tunampongeza kwa ushindi huo. Ila anatakiwa atoe ushirikiano kwa kila mmoja bila kujali chama kwa masilahi ya jimbo letu," amesema Magirwa Peter Agathon aliyekuwa mgombea kupitia chama cha DP.

Naye Ali Fikirini Liwali aliyekuwa mgombea wa CUF, amesema hawana shaka na ushindi alioupata mwenzao, hivyo wanatakiwa kuwa kitu kimoja kwa masilahi ya wananchi.

Tags: CCMFuoniUbungeYashinda
TNC

TNC

Next Post

Mbaroni kwa tuhuma za kuteka lori la mizigo

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company