Thursday, January 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Anaswa akitupa kichanga kwenye paa la nyumba

by TNC
December 29, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Polisi Wamshikilia Msaidizi wa Nyumbani Kwa Kutupa Kichanga Mwanza

Mwanza – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia na linaendelea kumuhoji Fahima Twaibu (19), msaidizi wa kazi za nyumbani kwa tuhuma za kutupa kichanga chenye jinsia ya kike, kinachokadiriwa kuwa na saa mbili tangu kuzaliwa.

Msaidizi huyo wa kazi za nyumbani mkazi wa Mtaa wa Balyehela wilayani Ilemela anadaiwa kufanya tukio hilo Desemba 25, 2025 saa 11.00 alfajiri.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 29, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, mtuhumiwa Fahima Twaibu anadaiwa kutupa kichanga hicho muda mfupi baada ya kujifungua kwenye paa la nyumba inayomilikiwa na Emmanuel Muruli, ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma na mkazi wa Balyehela.

Mutafungwa amesema askari polisi walifika eneo hilo na kufanikiwa kuokoa maisha ya kichanga hicho kwa kushirikiana maofisa wa ustawi wa jamii pamoja na wananchi wa eneo hilo, na kukifikisha katika Hospitali ya Mkoa Sekou-Ture kwa matibabu.

"Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa ikiwemo kufikishwa mahakamani. Vitendo vya ukatili kwa watoto ni kosa la jinai na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo," amesema Mutafungwa.

Ameongeza kusema kuwa, "tunatoa wito kwa jamii kushirikiana kwa karibu katika kulinda haki na maisha wa watoto kwa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi yao."

Wapenzi Wawili Wafariki Kwa Sababu ya Wivu wa Mapenzi

Katika tukio lingine, watu wawili ambao ni wapenzi wamefariki dunia baada ya kuzuka ugomvi ambao ulisababishwa na wivu wa mapenzi.

Wilbert Yona (34), mfanyakazi wa kiwanda cha Ziwa Steel na mkazi wa Kata ya Ihayabuyaga, anadaiwa kumuua mpenzi wake, Marietha Kalafala (33), mfanyakazi katika Kiwanda cha Ziwa Steel na mkazi wa Mwabuyi, kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kisha na yeye kujinyonga.

Tukio la mauaji ya Marietha Kalafala lilitokea Desemba 27, 2025 saa 2.15 usiku, katika Kitongoji cha Mwabuyi Kata ya Nyanguge wilayani Magu, aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni, mgongoni na kwenye paji la uso kisha mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi.

Mutafungwa amesema baada ya ufuatiliaji ndipo Desemba 28, 2025 saa 3.00 asubuhi katika nyumba ya kulala wageni, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa mmiliki wa nyumba hiyo kuwa kuna mteja wao amejiua kwa kujinyonga kwenye chumba alichokuwa amekodi.

"Baada ya askari polisi kufika kwenye nyumba hiyo mwili wa mtu huyo ulitambuliwa kuwa ni Wilbert Yona, aliyekuwa anatafutwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Marietha Benjamini Kalafala," amesema Mutafungwa.

Amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Lugeye Wilaya ya Magu, kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu na uchunguzi utakapokamilika miili hiyo itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi.

"Chanzo cha matukio haya ni wivu wa mapenzi kwani inadaiwa Wilbert Yona alikuwa akimtuhumu Marietha Kalafala kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine," amesema Mutafungwa.

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi hususan wapenzi na wanandoa kuacha kujichukulia sheria mikononi wanapopata migogoro ya kimapenzi au ya kifamilia, badala yake watafute msaada wa ushauri kupitia watu wanaowaamini, ustawi wa jamii, viongozi wa dini au vituo vya huduma ya kisaikolojia.

Tags: akitupaanaswakichangaKwenyenyumbapaa
TNC

TNC

Next Post

Transport, power supply disrupted as heavy rains hit Tanzania

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company