Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mtu mmoja afariki, wengine watatu wajeruhiwa baada ya kugongwa na radi Tabora

by TNC
December 28, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kijana Mmoja Afariki, Wengine Wawili Wajeruhiwa Kwa Kupigwa na Radi Tabora

Tabora – Kijana mmoja aitwaye Mwagala Malando (19), mkazi wa kata ya Itambilo wilayani Kaliua mkoani Tabora, amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa kwa kupigwa na radi.

Akizungumza Desemba 28, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema watu hao wamepigwa na radi wakati wamejikinga na mvua kwenye baraza mbele ya nyumba yao.

"Walikuwa wamesimama mbele ya nyumba yao kuna baraza hivi iliyotengwa na mti kwa muda wakati mvua kubwa inanyesha wakapigwa na radi, mmoja akafariki wawili wakajeruhiwa," amesema.

Waliojeruhiwa na radi hiyo ni Yohana Peter (18) na George Deus (18) wote wakazi wa Kijiji cha Itambilo wilayani Kaliua, ambapo wameshapatiwa matibabu na kurejea nyumbani wakiuguza majeraha.

Onyo la Tahadhari kwa Wananchi

Kamanda Abwao amewasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ili kuepuka majanga kama hayo ikiwa ni pamoja na kuacha kusimama chini ya miti wakati mvua inanyesha na kuacha kutumia vitu vinavyoweza kusababishiwa shoti wakati radi inapiga.

Juma Makola, mkazi wa Tabora amesema wakati mvua zikiwa kubwa Tabora kunakuwa na radi nyingi ambapo mara kadhaa hupiga mifugo na watu.

"Naiomba Serikali kama kuna elimu ya kujikinga na majanga ya radi wananchi wapewe ili kujikinga maana radi zinatokea mara nyingi kila ifikapo mvua za masika Tabora lazima baadhi ya watu au mifugo lazima waumie na radi," amesema.

"Tumeshajua kabisa ikifika masika tunaulizana safari hii atapigwa nani na radi maana Tabora radi zinaanguka sana, lakini tungejua kama kuna njia tunaweza kutumia tukaepukana na hayo majanga, kwa kweli tuelekezwe maana radi zinatuumiza sana," aliendeleza.

Wananchi Waomba Elimu ya Usalama

Mwajuma Seif, mkazi wa Tabora, amesema kuna wakati mtu anaogopa hata kukinga maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa sababu ya kuhofia kuumizwa na radi, lakini pia hasara za vifaa mfano luninga zinaungua sana.

"Radi zikianza tu tunahangaika kuzima simu, kuzima TV na kila kitu tunachohisi huenda kikaleta shoti, kwa sababu tunaogopa na ndio hivyo tushaona wenzetu baadhi wamepigwa radi wameumia wengine wamefariki dunia wameacha familia zinahangaika," amesema Mwajuma.

Tags: afarikiBaadakugongwaMmojaMtuRadiTaboraWajeruhiwaWatatuWengine
TNC

TNC

Next Post

Hutaki mtoto wako awe mnafiki? fanya haya

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company