Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wawili wakutwa na kesi ya kujibu, wakituhumiwa kusafirisha bangi

by TNC
December 24, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu Kulwa Mathias na mwenzake Edina Paul, wanaokabiliwa na shtaka la kusafirisha bangi.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuanza kujitetea Desemba 29, 2025.

Mathias na Edina wanakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa gramu 512.50.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo Mei 11, 2024 eneo la ukaguzi wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, kinyume cha sheria.

Uamuzi huo umetolewa Jumatano Desemba 24, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao wa mashahidi 12 na vielelezo 11.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Adolf Verandumi akishirikiana na Neema Kabodya waliieleza Mahakama hiyo kuwa kesi imeitwa kwa ajili ya usikilizwaji.

Baada ya shahidi wa 12 kumaliza kutoa ushahidi wake, upande wa Jamhuri ulifunga ushahidi wake na mahakama ilipitia ushahidi wa mashahidi hao wa upande wa mashtaka na kuwakuta washtakiwa kuwa wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa hao baada ya kukutwa na kesi ya kujibu, walidai kuwa watajitetea wenyewe kwa njia ya mdomo na hawatakuwa na shahidi wala kielelezo.

Hakimu Makube baada ya kusikiliza maelezo ya washtakiwa, aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 29, 2025 kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Machi 5, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 5543 ya mwaka 2025.

Tags: bangikesiKujibukusafirishawakituhumiwawakutwaWawili
TNC

TNC

Next Post

President calls for bold shift to modernise Zanzibar's towns

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company