Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watanzania hawashabikii haki, siyo wadau wa haki – Askofu Ruwa’ichi

by TNC
December 24, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Askofu Mkuu Ruwa’ichi: Watanzania Wengi Hawashabikii Haki

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa’ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki.

Amesema wengi wao kwa ujinga, kwa kurubuniwa au vinginevyo wamekuwa wadau wa amani akiweka msisitizo kuwa pasipo na haki hakuna amani.

Askofu Ruwa’ichi ametoa kauli hiyo leo Desemba 24, 2024 katika misa maalumu ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

"Sisi tunaoadhimisha Krismasi kuzaliwa kwa mwokozi tunatakiwa kuwa watu wa haki, wewe mwana Dar es Salaam, Mtanzania je, wewe ni mtu wa haki…? Wewe ni mdau wa haki….? Naomba kuthubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki siyo wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani," amesisitiza.

Askofu Ruwa’ichi ameeleza kuwa hana ugomvi na mtu anayeshabikia amani lakini akiwakumbusha kuwa haiwezekani kuwepo kwa amani bila haki.

Amesema haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana na vyote hivyo ni zawadi inayofunganamana na Yesu mwokozi.

"Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na yanayompendeza Mungu," amesema.

Askofu huyo amehitimisha mahuburi hayo akisema Yesu Kristo aliyezaliwa kwa ajili ya wanadamu anatambulika kwa haki, mwokozi, mwenye upendo na huruma.

Akizungumzia mafundisho hayo muumini wa kanisa hilo, Barnaba Josephat amesema hitaji la haki ni la msingi kwa binadamu kwa kuwa bila haki hakuna amani.

"Amani msingi wake mkuu ni haki, ukitenda haki amani lazima itakuwepo kwahiyo nimejifunza viongozi wetu wa kiroho wanatutaka tusimamie haki na kutoumiza watu wengine, unaweza kuishi katika utulivu lakini huna amani kwa sababu hujatendewa haki," amesema.

Kwa upande wake, Lightness Samson amesema katika kusheherekea Sikukuu za Krismasi ni muhimu Watanzania kuendelea kutenda mema pamoja na kutenda haki.

"Tuishi kwa umoja na upendo kwenye jamii tuilinde amani yetu kwa kutenda haki," amesema.

Tags: AskofuHakihawashabikiiRuwaichiSiyoWadauWatanzania
TNC

TNC

Next Post

Waathirika wa ajali ya helikopta Mlima Kilimanjaro wametambuliwa

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company