Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Tume ya Utumishi yakubali rufaa 15, ikitaja makosa matano

by TNC
December 23, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

TUU Yakubali Rufaa 15 kati ya 88, Yataja Makosa Matano Makuu

Dodoma – Tume ya Utumishi wa Umma (TUU) imekubali rufaa 15 kati ya 88 zilizoombwa, ikitaja makosa matano yanayolalamikiwa zaidi katika utumishi wa umma.

Makosa hayo ni utoro kazini, wizi na rushwa kwa mali ya umma, kughushi vyeti na taarifa za uongo, kukiuka maadili, uzembe uliosababisha hasara kwa Serikali na uzembe wa kushindwa kutekeleza majukumu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jumanne Desemba 23, 2025, Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Umma, John Mbisso, amesema makosa hayo yamebainika katika mkutano wa pili uliomalizika hivi karibuni mjini Morogoro.

Huu ulikuwa mkutano wa pili kwa mwaka huu wa fedha ambao ulifanyika Manispaa ya Morogoro chini ya Mwenyekiti wa TUU, Jaji mstaafu Hamisa Kalombola.

Mbisso amesema makosa hayo yalichomoza kwa wingi kwenye malalamiko, hivyo yalionekana kutendwa zaidi na watumishi wa umma.

"Kwa upande wa malalamiko, mengi yaliyowasilishwa na kuamuliwa na Tume yalihusu kupinga watumishi kutolipwa stahiki zao na waajiri, ikiwemo mishahara, stahiki za uhamisho na posho mbalimbali zitokanazo na kutekeleza majukumu yao," amesema.

Ametaja malalamiko mengine ni kuondolewa kwenye utumishi wa umma kinyume cha sheria na kusitishwa kwa ajira kinyume cha sheria.

Mbisso amesema watumishi 15 rufaa zao zilishinda moja kwa moja, wakati 14 walikubaliwa kwa masharti maalumu.

Kwa idadi hiyo, jumla ya watumishi 49 wamenufaika kwa mwaka huu wa fedha kurudishwa kazini, waajiri wakiagizwa kutoa haki kwa watumishi hao, ikiwamo kulipwa stahiki zao.

Ofisa wa Tume ya Utumishi wa Umma, Hussein Mussa amesema watumishi 15 si kwamba wote walikuwa wamefukuzwa na waajiri wao bali ndani ya rufaa hizo wengine walikuwa na rufaa za kuondolewa madaraja na kusimamishiwa mishahara.

Amesema siyo rufaa zote zinazopelekwa mbele ya Tume ni za watu kufukuzwa kazi, kwani wengine hupeleka malalamiko kutokana na kupunguziwa mishahara, kushushwa vyeo na wengine kuwa na barua za onyo bila sababu za msingi.

"Kwa hiyo tunaposema rufaa zimekubakiwa ni pamoja na makundi hayo na kwa namna yoyote mtu akishinda inabidi arudishiwe haki na stahiki zake zote ambazo alishazipoteza au kunyang’anywa," amesema.

Tags: ikitajaMakosaMatanoRufaaTumeutumishiyakubali
TNC

TNC

Next Post

Tourism body urges reforms amid expansion of airports

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company