Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mikoa yapewa agizo la kuchunguza manunuzi ya umma

by TNC
December 22, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu Aagiza Mikoa Kuanzisha Vitengo vya Uchunguzi wa Manunuzi na BQ

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba, ameelekeza mikoa yote nchini kuanzisha vitengo maalumu vya kuchunguza taratibu za manunuzi na BQ badala ya kusubiri mbio za Mwenge wa Uhuru, hatua inayolenga kulinda ustawi wa huduma na matumizi sahihi ya fedha za umma.

Dk Mwigulu amesema takribani asilimia 70 ya bajeti ya Serikali hutumika kwenye manunuzi na ujenzi, hivyo ni lazima mifumo ya usimamizi iimarishwe ili kulinda fedha zinazotokana na kodi za Watanzania.

Dk Mwigulu ametoa maelekezo hayo leo Desemba 21, 2025, alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Nachingwea, mkoani Lindi.

"Naagiza kila mkoa uwe na vifaa na wataalamu wanaoweza kubaini kama taratibu za manunuzi zimefuatwa bila kubomoa majengo. Tuko kwenye maandalizi ya bajeti, hivyo ni muhimu kuwa na wataalamu wa kukagua majengo ya aina hii," amesema Dk Mwigulu.

Ameeleza kuwa Serikali imechoshwa na tabia ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa wataalamu wa kuchunguza BQ na kulinganisha kilichoandikwa na kazi halisi iliyotekelezwa.

"Jengo linaweza kupakwa rangi na kuonekana zuri, lakini bila BQ huwezi kujua kama thamani ya fedha imezingatiwa. Nataka kila mkoa uwe na kitengo na vifaa vya kuchunguza majengo bila kusubiri mbio za Mwenge wa Uhuru," amesema.

Amesema katika uchunguzi wake amebaini kuwa kipindi cha mbio za Mwenge wa Uhuru huchaguliwa miradi michache iliyo bora ili mikoa ipate sifa, hali inayoficha mapungufu katika miradi mingine.

"Haiwezekani tujitungie mtihani wetu wenyewe halafu tukose makosa. Vitengo hivi vitafuatilia kila jengo ili kubaini maeneo ambayo serikali imetoa fedha lakini hazikutumika ipasavyo," amesema.

Amesisitiza kuwa anapotembelea miradi anahitaji kupata taarifa za BQ, fedha zilizotumika na kama zinalingana na kazi iliyofanyika, akibainisha kuwa Serikali inataka thamani ya fedha ionekane wazi katika kila mradi.

Pia ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kufanya tathmini ya miradi yote waliyopewa fedha ili kuhakikisha imetekelezwa kwa kuzingatia BQ, akisema kuwa huo ni msingi wa ugatuaji wa madaraka na uwajibikaji.

Baada ya maagizo hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisem), Reuben Kwagilwa, amesema ofisi yake itayasimamia kikamilifu maagizo hayo.

"Umetoa maelekezo kwa upande wa Tarura, Waziri Mkuu, nakuhakikishia tutayasimamia," amesema Kwagilwa.

Tags: agizoKuchunguzaManunuzimikoaUmmayapewa
TNC

TNC

Next Post

Mdau ataja ugumu wa utekelezaji wa gridi ya Taifa ya maji, aonyesha njia

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company