Sunday, January 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mpogolo avutiwa mabadiliko jina jipya chemba ya biashara

by TNC
December 21, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Uzinduzi wa Jina na Nembo Mpya ya Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC)

Dar es Salaam – Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema mabadiliko ya jina la Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), ni hatua ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa na kufikia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Akizungumza Jumapili Desemba 21, 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa mabadiliko ya jina la Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na kuzindua nembo mpya ya TNCC, Mpogolo amesema hatua hiyo inaakisi mageuzi ya kimfumo na kiuendeshaji yatakayoiwezesha TNCC kuwa taasisi imara, shindani na yenye sauti ya kuaminika kwa wafanyabiashara ndani na nje ya nchi.

Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza kuwa sekta binafsi ni mhimili muhimu wa maendeleo ya kiuchumi na Serikali kwa kulitambua hilo, itaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa TNCC, Vicent Minja amesema mabadiliko hayo yanafungua zama mpya za kuimarisha uwakilishi wa wafanyabiashara, kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana, pamoja na kukuza mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TNCC, Oscar Kissanga amesema mabadiliko ya jina na nembo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na kuimarisha ushindani wa wafanyabiashara wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Wakizungumzia hatua hiyo ya uzinduzi wa nembo mpya, wadau wa sekta ya biashara nchini, akiwemo Happy Simbeye amesema hatua hiyo inaweza kufungua ukurasa mpya wa mwelekeo na uongozi wa chemba hiyo.

Tags: avutiwaBiasharachembajinajipyaMabadilikoMpogolo
TNC

TNC

Next Post

Polisi Dodoma wanakanusha kumkamata Katibu wa Chadema kanda ya kati

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company