Thursday, January 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Utalii wa usiku kuvutia watalii Tarangire

by TNC
December 19, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Utalii wa Usiku na Tembo Pacha Kuvutia Wageni Zaidi Tarangire

Tarangire – Hifadhi ya Taifa ya Tarangire inatarajia kuongeza idadi ya watalii kupitia uanzishwaji wa utalii wa usiku, kivutio kipya kinachokamilisha uzoefu wa watalii wanaokuja kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha, kivutio kingine kipya ni kutambua tembo wanaozaa pacha, ambapo mchakato wake upo katika hatua za utafiti, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii na kuchangia kukuza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa Ijumaa, Desemba 19, 2025 na ofisa uhifadhi anayeshughulikia masuala ya utalii katika hifadhi hiyo.

Ofisa huyo amesema utalii mpya wa usiku utaongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi, hatua inayotokana na jitihada za Serikali za kutangaza na kuanzisha mazao mapya ya utalii nchini.

Kuhusu tembo wanaozaa pacha, ofisa huyo amesema suala hilo linaendelea katika mchakato wa tafiti mbalimbali ili kuhakikisha taarifa sahihi zinapatikana.

Mmoja ya waongoza watalii, Luka Pallangyo amesema katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka watalii wengi hupendelea kutembelea hifadhi mbalimbali, baadhi wakiwa na familia zao.

"Wageni wengi wanapenda mazingira na tunapoelekea mvua inanyesha, hivyo kunakuwa na mandhari ya kijani inayovutia zaidi," amesema.

Watalii Wapongeza Vivutio vya Tanzania

Mmoja wa watalii kutoka Marekani, Kelly Anderson, amesema Tanzania ni nchi yake ya 10 barani Afrika kutembelea na amevutiwa na mandhari katika Hifadhi za Taifa za Serengeti na Tarangire na ukarimu wa Watanzania.

Amesema mwaka huu amekuja kutembelea hifadhi mbalimbali hapa nchini katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa na kuwa anatarajia kurudi mwakani tena kutembelea vivutio vingine.

"Kiukweli kwa namna nimeona hifadhi hizo, nimeona wanyama na mandhari ya kuvutia nzuri zaidi ya inavyoonekana kwenye picha. Kuna uzuri wa asili na nimejihisi kama niko nyumbani nikiwa hapa Tanzania," amesema.

"Tanzania ni nchi ya 10 Afrika na nina tamani kutembelea nchi zote 54 za Afrika ila kabla sijaendelea na nchi zingine lazima nirudi Tanzania mwakani, kwani ninajiona niko nyumbani," aliongeza.

Naye Janine Hellwig kutoka Ujerumani, amesema katika Hifadhi za Taifa za Ziwa Manyara na Tarangire ambazo wametembelea, wamejionea wanyama wa aina mbalimbali.

"Tumefurahi sana kwani tumeona wanyama wengi wakiwemo chui, tembo, twiga, viboko, nyati na wengine, tunaamini tunapoendelea kwenye hifadhi nyingine tutajionea wanyama wengine zaidi na vivutio vingine vilivyopo Tanzania," amesema.

Tags: kuvutiaTarangireUsikuutaliiWatalii
TNC

TNC

Next Post

Kariakoo bustles amid festive season shopping rush

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company