Saturday, January 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Elimu ya historia itolewe kwa ubunifu, teknolojia

by TNC
December 19, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Chama cha Wanahistoria Tanzania Chatakiwa Kusambaza Elimu kwa Jamii

Dodoma – Chama cha Wanahistoria Tanzania (HAT) kimetakiwa kusambaza elimu, utafiti na ubunifu wa kihistoria nchini badala ya kuuacha kwenye makaratasi bila jamii kunufaika nao.

Wito huo umetolewa Ijumaa Desemba 19, 2025 na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Revocatus Bugumba kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

Bugumba amesema kuwa Tanzania imejenga uhusiano wa kimataifa kupitia matukio ya kihistoria na urithi wa kiutamaduni, hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo chanya ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Amesema uendelezaji wa historia unachukua nafasi muhimu katika kuimarisha mahusiano ya kimataifa.

"Tukifanya tafiti ni muhimu zirudi kwa jamii husika kwa sababu ni kumbukumbu ya alama na utambulisho wao, pia katika kupambana katika kipindi hiki cha utandawazi na mabadiliko ya teknolojia ili historia iendelee kuwa utambulisho wa Taifa," amesema.

Bugumba ameongeza kwamba yote yakiwezekana, inasaidia kujenga umoja wa kweli na kuhamasisha kizazi kijacho kiweze kuipenda historia yao.

"Hivi sasa kuna somo la Historia ya Tanzania na Maadili linalofundishwa shuleni ambalo ni jambo jema ili watoto wathamini walikotoka na waweze kuendana na teknolojia," alisema.

Upotoshaji wa Taarifa za Kihistoria

Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Ali Mkubwa amesema kumekuwa na upotoshaji wa baadhi ya taarifa za historia nchini, hivyo ni lazima kufanyika utafiti wa kina ili kuboresha maeneo ya historia.

Dk Mkubwa amesema ni jukumu la HAT kuhakikisha wanafanya utafiti wa kutosha katika maeneo ya kihistoria nchini na kuja na taarifa sahihi zitakazoelimisha Watanzania kuhusu historia ya maeneo yao.

Historia ni Nembo ya Taifa

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanahistoria nchini, Profesa Maximillian Chuhila amesema historia ni nembo ya Taifa na urithi wa utamaduni wenye kuitambulisha Tanzania, hivyo ni muhimu watu wakaijua.

Profesa Chihila amesema kila Taifa duniani lina historia yake, hivyo Watanzania ni lazima wajivunie historia yao ambayo ni urithi na utambulisho kila wanapokwenda.

Ameipongeza Serikali kwa kuanzisha somo la Historia ya Tanzania na Maadili kwa wanafunzi kwani itasaidia vijana wengi kujifunza na kuifahamu historia ya nchi yao na kuachana na kuiga utamaduni wa kigeni.

Tags: ElimuHistoriaitolewekwaTeknolojiaUbunifu
TNC

TNC

Next Post

Serikali yatoa agizo juu ya matumizi sahihi ya mapato ya MBOMIPA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company