Thursday, January 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Tanzania yajibu zuio la Marekani

by TNC
December 17, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imejibu uamuzi wa Marekani kuiweka nchi katika kundi la mataifa 15 yaliyowekewa uthibiti wa visa vya kuingia nchini humo, ikisema itaendelea na mazungumzo ya kidiplomasia ili kupata muafaka unaolinda maslahi ya wananchi wa pande zote.

Kupitia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyotolewa leo, Desemba 17, 2025, Tanzania imeeleza kuwa hatua hiyo iliyotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, Desemba 16, 2025, inahusisha pia nchi nyingine 14 za Afrika, zikiwamo Nigeria, Senegal, Zambia na Zimbabwe.

Serikali ya Marekani imeeleza kuwa udhibiti huo umetokana na taarifa ya ukaaji wa zaidi ya muda, ikionesha baadhi ya raia wa Tanzania kuzidisha muda wa kukaa kinyume na masharti ya viza kwa viwango vya asilimia 8.30 kwa viza za B-1/B-2 na asilimia 13.97 kwa viza za F, M na J.

Hata hivyo, Serikali imesisitiza kuwa zuio hilo si kamili, na kwamba Watanzania watakaokidhi vigezo wataendelea kupewa ruhusa ya kuingia Marekani, huku ikiwahimiza wasafiri kuzingatia masharti ya viza ili kuepusha madhara binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

TNC itaendelea kukupatia taarifa za hivi karibuni kuhusu masuala haya.

Tags: MarekaniTanzaniayajibuzuio
TNC

TNC

Next Post

Tanzania turns to diplomacy after US travel restrictions

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company