Saturday, January 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwanahabari Arusha afariki dunia

by TNC
December 17, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mwanahabari Mkongwe Neema Mhando Afariki Dunia Arusha

Arusha. Tasnia ya habari Mkoa wa Arusha imepata pigo baada ya mwanahabari mkongwe, Neema Mhando (53) kufariki dunia Jumatano, Desemba 17, 2025 nyumbani kwa wazazi wake eneo la Daraja Mbili jijini Arusha.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Ofisa Habari wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Ally Nyambi kwa waandishi wa habari akisema Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji na watumishi wote wamepokea kwa masikitiko kuondokewa ghafla na mtumishi mwenzao.

"Kwa masikitiko makubwa nawajulisha mwandishi mwenzetu, Neema Mhando amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano.

"Jana tulikuwa naye ofisini ilipofika saa tisa alasiri dereva wa nyumbani kwao alikuja kumchukua na alipofika nyumbani kwao alikuwa chini ya uangalizi wao kisha alikwenda kujipumzisha na ilipofika saa 11 alfajiri alifariki," amesema Nyambi.

Neema hadi umauti unamkuta alikuwa Ofisa Habari Daraja la Pili wa Halmashauri ya Jiji la Arusha nafasi aliyoitumikia kwa kipindi cha miaka mitatu akitokea Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kilichopo Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.

Pia, aliwahi kufanya kazi Shirika la Utangazi Tanzania (TBC).

Baba mzazi wa marehemu, Profesa Peter Mhando akizungumza na TNC nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ameeleza kusikitishwa na msiba wa ghafla uliotokea na kuacha pengo kubwa katika familia hiyo.

"Familia imepokea msiba huu kwa maumivu makubwa, kila kitu tunamwachia Mungu, Neema alikuwa kipenzi cha kila mtu kwenye familia hii, tunamwomba Mungu aipumzishe roho yake mahali pema," amesema Profesa Mhando.

Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC), Claud Gwandu ameeleza kupokea taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwa masikitiko na kuwa waandishi wa habari waliofanya naye kazi wataendelea kumkumbuka kwa weledi na moyo wake wa kuwasaidia waandishi wanaochipukia kwenye taaluma ya habari.

"Neema alikuwa rafiki wa waandishi wa habari wakati akiwa Ofisa Habari Chuo Kikuu cha Nelson Mandela na alipohamia Halmashauri ya Jiji la Arusha ni mtu aliyekuwa akitoa ushirikiano kwa jambo lolote lililohitaji mchango wake, tumepoteza mtu aliyekuwa anatoa mchango muhimu kwenye tasnia yetu," amesema Gwandu.

Mwandishi Veronica Mheta amesema alimfahamu Neema Mhando tangu mwaka 2005 jijini Dar es Salaam kwenye majukumu ya habari akimwelezea ni mwanataaluma aliyependa kujifunza na kuwasaidia waandishi wachanga kufanya kazi zao kwa weledi.

Tags: afarikiArushaduniaMwanahabari
TNC

TNC

Next Post

Government urges private sector to tap into aviation investment opportunities

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company