Friday, December 12, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Abiria 40 wanusurika, basi likiteketea kwa moto Morogoro

by TNC
December 9, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Abiria 40 Waokoka Baada ya Basi Kuteketea Moto Morogoro

Morogoro. Abiria 40 wamenusurika baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda wilayani Malinyi mkoani Morogoro kuteketea kwa moto katika eneo la Maseyu mkoani hapa.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi, Desemba 9, 2025, katika kona kali ya Maseyu, Kata ya Gwata ambapo basi hilo aina ya Tata lilianza kuwaka moto na kuungua lote huku abiria wakifanikiwa kutoka wakiwa salama.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amesema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Halfan Omary, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, na lilikuwa limepakia abiria 40 ambao wote wameokolewa bila majeraha.

"Hili gari limeteketea kabisa, lakini tunashukuru hakuna abiria aliyejeruhiwa. Hata hivyo, mizigo na mali nyingine za abiria zilizokuwamo ndani zimeungua," amesema Kamanda Mkama.

Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya mfumo wa umeme wa gari, ingawa uchunguzi wa kina unaendelea kubaini undani wa tatizo hilo.

Kamanda Mkama ametoa wito kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya usafiri kuhakikisha magari yao yanapatiwa ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara, hususan yale yanayobeba abiria, ili kuepusha majanga yanayoweza kuhatarisha maisha ya watu na kuharibu mali.

Tags: AbiriabasikwalikiteketeaMorogoroMotowanusurika
TNC

TNC

Next Post

WHO warns rising antimicrobial resistance is undermining decades of medical progress

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company