Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mama na bintiye wateketea kwa moto Tabata

by TNC
December 2, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mama na Mtoto Wafariki Dunia Katika Moto wa Nyumba Tabata

Dar es Salaam. Mama na mtoto wake wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto, mtaa wa Nchimbi Tabata, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lililotokea saa 5 usiku wa Jumatatu, Desemba 1, 2025 limethibitishwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Peter Mabusi.

Tukio hilo limetokea katika makazi yenye nyumba mbili ambapo moja kubwa inakaliwa na mwenye nyumba Mary Mapunda na nyumba ndogo iliyoko nyuma, ilikuwa ikikaliwa na mpangaji aliyefariki dunia, Latifa Maseta.

Wananchi Walijitahidi Kuokoa Uhai

Kwa mujibu wa Kamanda Mabusi, moto ulianzia kwenye nyumba ndogo ya mpangaji, ambayo ni chumba na sebule na vyote vimeteketea kwa moto.

"Wananchi wa jirani ndiyo waliokuwa wa kwanza kuona moshi na moto ukitoka nyuma. Mwenye nyumba hakusikia kabisa tukio likiendelea. Majirani baada ya kuona moto mkubwa walikimbia hadi eneo la tukio na kujaribu kuvunja mlango, lakini moto ulikuwa umeshika kasi wakashindwa kuingia," amesema Mabusi.

Miili Yapatikana Imeungua

Mabusi amesema baada ya kikosi cha zimamoto kufika, walifanikiwa kuuzima moto na kuingia ndani ambapo walikuta miili ya Latifa, mwenye umri unaokadiriwa kati ya miaka 30 hadi 35, na mtoto wake wa kike Alice, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 hadi 12.

"Wote walikuwa wameungua vibaya na walishafariki, kwa taarifa za awali, inaonekana tukio hili linaweza kuwa si la kawaida, lakini pia kuna madai mlango ulikuwa umefungwa kwa nje wakati majirani walipofika. Hatuwezi kuthibitisha chochote kwa sasa hadi uchunguzi ukamilike," amesema.

Uchunguzi Unaendelea

Amesema uchunguzi wa wataalamu wa zimamoto pamoja na vyombo vingine vya dola utaendelea ili kubaini chanzo halisi cha moto na mazingira yaliyosababisha vifo hivyo.

Rafiki wa marehemu amesema siku ya tukio walikuwa na marehemu Latifa baa iliyopo jirani na alipokuwa anaishi, na ilipofika saa tano usiku aliaga kurudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo.

"Tulikuwa naye jana usiku, baadaye akasema anaenda kumuangalia binti yake na kubadilisha nguo kisha angerudi tena kuungana na sisi lakini ghafla tukasikia kelele za moto," amesema.

Amesema kutokana na kelele kuwa kubwa walifika eneo la tukio na kukuta vyumba vya Latifa vikiteketea kwa moto na yeye akiwa ndani na mtoto wake na baada ya kuzimwa walikutwa wamegandana.

"Hatujui chanzo nini lakini imetuumiza marafiki zake kwani tulikuwa naye muda mchache kabla ya kifo chake, huyu dada hakuwa na ugomvi maana alikuwa anajishughulisha na uuzaji wa nyama eneo la Kibo," amesema.

Mwenye Nyumba Azima Umeme

Kwa mujibu wa mmiliki wa nyumba, Mary Mapunda amesema alisikia kelele za moto kutoka kwa mpangaji wake mwingine hivyo kuchukua uamuzi wa kuzima switi kuu ya umeme.

"Nilikuwa nimelala ndani, ghafla nikasikia mpangaji mwingine ambaye yupo jirani na vyumba vyangu akipiga kelele. Niliposikia anaita moto nilishtuka nikatoka chumbani," amesema Mary.

Amesema baada ya kutoka nje, jambo la kwanza alikimbilia kuzima swichi kuu ya umeme na kwenda chumba cha wajukuu zake kuwatoa nje.

"Niliwatoa haraka tulipotoka nje ndipo nikakuta moto tayari umesambaa kwa kasi, tukaendelea kupiga kelele za msaada kwa majirani walikuja wakaanza kumwaga maji kuuzima na baadaye kikosi cha zimamoto kilifika, lakini tayari moto ulikuwa umeshadhibitiwa na wananchi," amesema Mary.

Mary amesema hawezi kusema kama moto umetokana na hitilafu ya umeme au jambo jingine, kwani mwanzoni alikuwa ameshazima ‘main switch’ kabla ya moto kusambaa zaidi.

"Siwezi kusema ni umeme, siwezi kusema ni kitu kingine, hatukujua chanzo kwa sababu nilivyosikia moto nilikimbilia kuzima umeme nyumba nzima," amesema.

Tags: bintiyekwamamaMotoTabatawateketea
TNC

TNC

Next Post

Man whose genitals were severed appeals for further medical help

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company