Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Baba amuua mwanaye wa miaka miwili kwa kumnyonga, kisha ajinyonga mwenyewe

by TNC
November 21, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mbeya: Baba Auwa Mtoto Wake wa Miaka Miwili Kisha Ajinyonga

Mbeya. Mtoto wa miaka miwili Deniva Derick (2) ameuwawa kwa kunyongwa hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila na Baba yake mzazi Derick Mwangama (23), ambaye naye alijinyonga na kupoteza maisha.

Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 18, 2025 katika Kijiji cha Isaka, Kata ya Nkunga, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya leo Novemba 21, 2025 amesema awali kabla ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo ambao wote ni marehemu, alikwenda nyumbani kwa mzazi kwenzie Violeth Edward (19) na kumchukua kwa nguvu mtoto huyo huku akiwa na jazba.

Kamanda amesema baada ya kuondoka naye, baadaye mwili wa mtoto ulikutwa ukiwa umenyongwa na kisha kutekelezwa kando ya Mto Kiwira.

Amesema baba wa mtoto huyo ambaye ni marehemu baada ya kufanya mauaji hayo ya mwanaye, alijinyonga kwa kutumia kamba ya manila kwenye mti wa parachichi kando ya mwili wa mtoto wake.

"Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni kuibuka kwa mgogoro baina wenza hao ambao walikuwa wametengana," amesema Kamanda wa Polisi.

Wito kwa Wazazi

Katika hatua nyingine Kamanda amesema amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka wazazi pindi wakiwa na migogoro ya kifamilia kutafuta njia sahihi ya kutatua kwa kushirikisha watu wa jirani ili kuepuka madhara kama hayo.

"Watu walio kwenye ndoa wajitahidi kuepuka migogoro kwa kutafuta njia sahihi ya kutatua kwa amani ili kuachana na uamuzi wa kujikatisha uhai," amesema.

Mkazi wa eneo hilo, Damian Haule amesema miaka ya sasa migogoro mingi ya kifamilia chanzo kikubwa ni wanawake wakimiliki uchumi mkubwa hudharau wenza wao na kubeba jukumu la kutunza na kuhudumia familia.

"Huku mitaani tunashuhudia hali siyo nzuri wanaume wana dhalilishwa na hata kutukanwa matusi ya nguoni na wenza wao jambo ambalo hupelekea kuchukua maamuzi magumu," amesema.

Mwananchi mwingine Erasto Mwakalonge amesema kimsingi miaka ya sasa ndoa zimekuwa chungu kwa wanaume hususani mwanamke akibarikiwa kuwa na uchumi kumzidi mwenza wake.

Tags: ajinyongaAmuuaBabakishaKumnyongakwaMiakamiwilimwanayemwenyewe
TNC

TNC

Next Post

Court of Appeal upholds ruling against cement company in tax dispute with revenue authority

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company