Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

15 waendelea kupeta naibu uwaziri, wengine 11 wapo

by TNC
November 18, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Naibu Mawaziri 15 Warejeshwa Nafasi Zao, Wengine Wapandishwa

Dar es Salaam – Kati ya Naibu Mawaziri 25 waliokuwepo katika Baraza la Mawaziri lililomaliza muda wake, 15 wamerejeshwa kutumikia nafasi hizo ingawa baadhi katika wizara tofauti, huku wengine wakipandishwa kuwa mawaziri.

Idadi hiyo, inafanya naibu mawaziri wasiorudishwa katika wadhifa huo, ifikie 11. Baadhi wamekosa sifa kwa sababu walishindwa kupenya kwenye kinyang’anyiro cha ubunge na wengine wamepewa nafasi nyingine nje ya muhimili wa Serikali.

Mbunge wa Mbinga Vijijini, Judith Kapinga anakuwa mmoja wa naibu mawaziri wa baraza lililopita, aliyeruka viunzi vya nafasi hiyo na sasa ni Waziri kamili.

Mwanazuoni huyo wa sheria, alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, lakini sasa amekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Nafasi hiyo ilikuwa chini ya Dk Selemani Jafo ambaye sasa si sehemu ya baraza la mawaziri.

Deus Sangu ameteuliwa kuwa Waziri katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Ukiacha Kapinga na Sangu, wapo naibu mawaziri waliorejeshwa kwenye nyadhifa hizo, tena katika wizara zilezile walizozitumikia katika baraza la Rais Samia Suluhu Hassan lililopita.

Wamerudishwa Wizara Zilezile

Miongoni mwa naibu mawaziri hao ni Ummy Nderiananga aliyekuwa katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu na sasa yupo wizara hiyohiyo iliyoongezewa na kipengele cha Wenye Ulemavu.

Sambamba na Ummy, mwingine ni Mbunge wa Tunduma, David Silinde aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo, chini ya Hussein Bashe na sasa amerejeshwa tena wizara humo. Lakini sasa atakuwa chini ya Daniel Chongolo.

Kundo Mathew naye amesalia kuwa Naibu Waziri wa Maji. Zaidi ya hayo Mbunge huyo wa Bariadi Mjini, anaendelea kuwa chini ya Jumaa Aweso kama ilivyokuwa katika baraza lililopita.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya ataendelea kushika wadhifa huo. Kasekenya pia, ataendelea kuwa chini ya Waziri wake, Abdallah Ulega.

Kama ilivyo kwa Kasekenya, ndivyo itakavyokuwa kwa David Kihenzile aliyekuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na sasa ameteuliwa tena kushika wadhifa huo, chini ya Profesa Makame Mbarawa.

Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA naye, amekuwa miongoni mwa naibu mawaziri waliorudishwa kuzitumikia nafasi walizokuwa nazo awali. Mbunge huyo wa Muheza, alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na sasa amerejeshwa wizara hiyo hiyo.

Zaidi Mwana FA atakuwa chini ya waziri yuleyule, Mbunge wa Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi. Pia, ameongezewa Paul Makonda kuwa Naibu Waziri mwenza katika wizara hiyo.

Wizara nyingine ambayo haijashuhudia mabadiliko katika nafasi ya Naibu Waziri ni Madini. Stephen Kiruswa anaendelea kushika wadhifa huo, huku wizara ikiongozwa na Anthony Mavunde kama ilivyokuwa kabla.

Wamerudi Lakini Wizara Tofauti

Katika orodha hiyo ya naibu mawaziri 15 walioteuliwa kuendelea na nafasi hizo, wamo waliorudishwa lakini si katika wizara walizozitumikia kabla.

Mbunge wa Wanging’ombe mkoani Njombe, Dk Festo Dugange ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira chini ya Hamad Masauni.

Awali, Dk Dugange alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia mambo ya afya.

Mwingine ni Dennis Londo ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Awali, Mbunge huyo wa Mikumi mkoani Morogoro, alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hali kama hiyo imemkuta Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Maryprisca Mahundi naye anaendelea kuwa naibu waziri. Lakini si katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Bali sasa atakuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, chini ya Dk Dorothy Gwajima.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameteuliwa kuendelea kuwa naibu waziri, lakini sasa ni katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Kigoma, Zainab Katimba naye ameendelea kuukwaa wadhifa wa naibu waziri. Lakini sasa sio tena katika wizara ya Tamisemi, bali ni Wizara ya Katiba na Sheria.

Kati ya naibu mawaziri waliokuwepo awali, Daniel Sillo amehamia katika muhimili wa Bunge. Sio kwa nafasi ya ubunge pekee bali amechaguliwa kuwa Naibu Spika.

Ukiacha Sillo, mwingine aliyekuwa naibu waziri ni Exaud Kigahe katika Wizara ya Viwanda na Biashara. Lakini, Mbunge huyo wa Mufindi si sehemu ya walioteuliwa sasa.

Pia, yumo Jumanne Sagini aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria. Kwa sasa si sehemu ya walioteuliwa katika nafasi hiyo kwa kukosa kigezo cha ubunge.

Sagini alishindwa kupenya katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Butiama. Katika mchakato wa kura za maoni CCM, Dk Charles Mahera ndiye aliyeongoza kwa kura na kuteuliwa kugombea na sasa ni mbunge wa jimbo hilo.

Dunstan Kitandula naye hayumo katika orodha ya walioteuliwa kuendelea na wadhifa huo. Kitandula alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, alishindwa katika kura za maoni za ubunge.

Mwingine aliyeachwa ni Alexander Mnyeti. Mbunge huyo wa zamani wa Misungwi, alishindwa kupenya katika kura za maoni na hivyo ameukosa ubunge.

Katika baraza la mawaziri lililopita, Mnyeti alikuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Utalii.

Kama ilivyo kwa Mnyeti, ndivyo ilivyotokea kwa Cosato Chumi aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hivyo, Chumi ameukosa ubunge na si sehemu ya baraza la mawaziri.

Wengine waliokumbwa na hali kama hiyo ni Omar Kipanga aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Geoffrey Pinda aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Khamis Khamis aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Pia, yumo Mwanaid Khamis aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Mwingine aliyekuwepo na sasa hayupo katika nafasi hizo ni Dk Godwin Mollel. Mollel aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, aliongoza katika kura za maoni na kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo.

Lakini, mbunge huyo wa zamani wa Siha bado si mbunge kwa sasa, baada ya uchaguzi jimboni humo kuahirishwa kutokana na kifo cha mmoja wa wagombea tena wa CUF.

Tags: kupetaNaibuuwaziriWaendeleawapoWengine
TNC

TNC

Next Post

Nactvet urges unqualified applicants to reapply

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company