Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Shule ya Sekondari Mkuu Rombo yateketea kwa moto

by TNC
October 28, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Bweni la Pili Lateketea Moto Shule ya Sekondari Mkuu Rombo

Rombo. Zikiwa zimepita siku 22 tangu bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mkuu, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro kuteketea kwa moto, bweni jingine la shule hiyo lenye wanafunzi 160 limeteketea tena kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumanne, Oktoba 28, 2025.

Tukio la kwanza lilitokea Oktoba 6, 2025, ambapo bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 90, linalomilikiwa na Kanisa Katoliki wilayani humo, liliteketea kwa moto wakati wanafunzi wakiwa kwenye ibada ya asubuhi.

Katika tukio hilo, mali zote za wanafunzi ziliteketea kwa moto ikiwemo magodoro 91, vitanda 46, nguo, madaftari na vifaa vingine vya matumizi binafsi.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema tukio hilo limetokea usiku wa Oktoba 27 na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, ingawa hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa.

"Tulipokea taarifa za moto katika bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkuu lililopo Kata ya Makiidi, Wilaya ya Rombo, tulifika haraka eneo la tukio na kukuta moto ukiendelea kuwaka ndani ya bweni. Askari wetu walifanya jitihada na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujasambaa zaidi," amesema Kamanda Mkomagi.

Kamanda Mkomagi amesema chanzo cha moto huo bado hakijabainika na uchunguzi unaendelea ili kubaini sababu hasa ya matukio hayo ya moto katika shule hiyo.

"Katika tukio hili hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa, lakini vitanda 89, magodoro 160, ofisi moja pamoja na madaftari ya wanafunzi vimeteketea kwa moto," amesema Kamanda Mkomagi.

Aidha, Kamanda Mkomagi ametoa wito kwa wananchi, taasisi za elimu na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto, na kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia namba ya dharura 114 pindi wanapobaini hatari ya moto.

Tags: kwaMkuuMotoRomboSekondariShuleyateketea
TNC

TNC

Next Post

Presidential candidate outlines five-year vision as party concludes campaign

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company