Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Makamu wa Rais atoa maoni kuhusu matukio ya Oktoba 29

by TNC
February 2, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Makamu wa Rais Nchimbi Atoa Onyo kwa Viongozi Wanaozungumzia Uchaguzi wa Oktoba 29

Dar es Salaam – Makamu wa Rais Dk Emmanuel Nchimbi amesema kitendo cha baadhi ya viongozi wa Serikali, taasisi za kijamii, vyama vya siasa na wanaharakati kuendelea kuzungumzia yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, nje ya mfumo wa kisheria uliowekwa juu ya jambo hilo, ni kutotendea haki taifa.

Dk Nchimbi amesema hayo leo Februari 2, 2026, alipozungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Sheria na kuanza kwa mwaka wa Mahakama 2026 jijini Dodoma, akiwa mgeni rasmi.

Makamu huyo wa Rais ametoa kauli hiyo akijibu ombi lililotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, aliyesema TLS inatambua yaliyojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi, na kwamba wanapendekeza kila anayehitajika kuwajibika awajibike kwa maslahi mapana ya Taifa.

"Katika kipindi hiki, tuwaombe hata viongozi wetu wenye dhamana, anapokuwa hana jambo muhimu sana la kuzungumza, asizungumze jambo ambalo litatonesha mioyo ya wananchi. Tuombe hekima kwa Mungu ili kulirejesha Taifa pamoja," amesema Dk Nchimbi.

"Hapa tulipo siko, na tusipokuwa makini huko tutakokwenda siko kabisa, tutafika mahali tutashindwa kurudi tulikotoka. Rai yetu ni kwamba tuangalie namna bora na shirikishi, yenye kuaminika na wote, na msingi wa kutuongoza katika hili iwe ukweli, haki, uwazi na uwajibikaji," ameongeza.

Wakili Mwabukusi amesema ni muhimu kama Taifa tuongee kwa ukweli, bila kufarijiana kwamba tumejitia aibu, lakini lazima itafutwe namna ya kutoka na njia hiyo iongozwe na ukweli, haki, uwazi na uwajibikaji.

Akijibu kauli hiyo, Dk Nchimbi amesema: "Sio vizuri kuzungumzia yaliyojiri Oktoba 29, 2025, kwa sababu yanatonesha kidonda na yanaweza yasisaidie kwenye mchakato wa haki."

"Kwanza, niseme nakubaliana naye kwa asilimia 100; pili, naongezea pale aliposahau, sio viongozi wa Serikali peke yake bali pia viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za kijamii na wanaharakati," amesema.

Dk Nchimbi amesema Rais Samia ameunda tume ya kufanya uchunguzi na inaendelea kufanya kazi, hivyo kuendelea kuzungumzia jambo hilo na wa viongozi wa Serikali, taasisi za kijamii na vyama vya siasa nje ya mfumo wa kisheria uliowekwa ni kutotendea haki taifa letu.

Amesema kila mtu anayeipenda Tanzania ni muhimu akubaliane kwamba watu wasitoneshane, bali vyombo vya kisheria vipewe nafasi kutimiza wajibu wao.

Tags: atoaKuhusuMakamuMaoniMatukioOktobaRais
TNC

TNC

Next Post

Ride-hailing company exits Tanzanian market after nearly a decade

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company