Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwigulu ahimiza ushirikiano katika utunzaji na uhifadhi

by TNC
January 31, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu Aagiza Ushirikiano wa Wadau katika Uhifadhi na Utalii

Arusha – Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, ameagiza wadau wa utalii, uhifadhi na Watanzania kushirikiana na kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya uhifadhi kwa maendeleo endelevu na uchumi wa taifa.

Aidha, amewataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini badala ya kutegemea watalii wa nje pekee.

Dk Mwigulu ameyasema hayo Jumamosi Januari 31, 2026, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Waziri Mkuu anatarajiwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika utoaji wa tuzo za utalii usiku wa leo.

Amesema kuwa jukumu la kusimamia uhifadhi siyo la Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pekee bali ni la wadau wote.

"Nitoe rai kwa wahifadhi na wadau kuhifadhi urithi huu ili na sisi tuwarithishe watoto wetu kama na sisi tulivyorithishwa; kila mmoja tuwajibike kuziendeleza lakini pia tutunze mazingira," amesema.

Dk Mwigulu ameongeza kuwa gharama za Watanzania ni Sh 11,800 ambazo anaziona kuwa ni nafuu na zinaweza kumudu. "Haimaanishi ni matajiri, lakini wameweka utaratibu wa kufanya kazi mwaka mzima na wametenga siku za kwenda kwenye maeneo kama haya kuondoa stresi," alisema.

"Utalii isiwe ni jambo la wageni toka nje ya nchi; ukishafanya kazi mwaka mzima, tenga sehemu ya kwenda kuona baraka hizi ambazo Mungu ametupa Watanzania. Wananchi pia mna wajibu wa kutunza rasilimali; si jambo la TANAPA peke yao. Hao tumewapa dhamana, lakini ni mali ya urithi kwa Watanzania—tutunze tuendelee kupata manufaa," aliendeleza.

Mmoja wa wadau wa utalii, Venance Lymo, amesema tuzo hizo zitaongeza thamani katika sekta hiyo na kutangaza Tanzania kimataifa katika utalii.

"Tuzo hizi zinaenda kuongeza thamani katika sekta ya utalii na kutangaza Tanzania kimataifa katika masuala ya utalii; zitahamasisha wawekezaji pia katika sekta hii muhimu inayoingizia Taifa letu mapato," amesema.

Tags: ahimizakatikaMwiguluuhifadhiUshirikianoUtunzaji
TNC

TNC

Next Post

Police launch crackdown on illegal bus lane users

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company