Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Polisi yamshikilia mwenyekiti wa chama cha siasa Mbeya Vijijini, yataja sababu

by TNC
January 23, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Polisi Mbeya Wamshikilia Mwenyekiti wa Chadema Wilayani Mbeya Vijijini

Mbeya – Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya Vijijini Getruda Lengesela kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwamo uchochezi.

Mtuhumiwa huyo anakamatwa ikiwa zimepita siku mbili tangu viongozi wengine wawili wa chama hicho, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa huo, Masaga Kaloli na Mwenyekiti wa Bavicha mkoani humo, Elisha Chonya kukamatwa na jeshi hilo kwa tuhuma kuhamasisha mkusanyiko isivyo halali.

Wawili hao walikamatwa Januari 21 katika Kijiji na Kata ya Inyala wakati Chadema ikijiandaa kuadhimisha miaka 33 ya kuzaliwa kwa Chama hicho, iliyokuwa imepangwa kuambatana na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na chakula ya pamoja.

Katika taarifa ya Jeshi la Polisi, ilieleza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakifanya maandalizi na kuhamasisha watu kukusanyika kufanya mkutano bila kufuata taratibu za kisheria.

"Ikumbukwe Chadema imezuiliwa na mahakama kufanya shughuli zozote za kisiasa, upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao" ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa iliyotolewa Januari 23 na Jeshi hilo, imesema mtuhumiwa amekamatwa Januari 22 saa 3:40 usiku katika eneo la Nsalala katika mji mdogo wa Mbalizi wilayani humo mkoani Mbeya.

"Anashikiliwa kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwamo uchochezi, upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake" imesema taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Mbeya, Hamad Mbeyale amesema huu ni mwendelezo wa viongozi wao kushikiliwa, akieleza kuwa bado hawatakata tamaa kwa mazingira wanayopitia.

Amesema haki ina gharama na inahitaji uvumilivu, akieleza kuwa kwa sasa wanafuatilia kujua hatma ya kiongozi huyo na wengine walioshikiliwa siku mbili zilizopita ili kuachiliwa huru.

"Niwaombe wananchi kuendelea kuvumilia, tunapitia vipindi vigumu ila ndio njia ya kuelekea kupata haki, gharama, muda na uvumilivu ni muhimu sana kwa wakati huu tunapolipambania Taifa" amesema Mbeyale.

Watuhumiwa Watatu Wakamatwa Kwa Dawa za Kulevya

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikiliwa watuhumiwa watatu Mseven Menat, Fred Lulandala na Joseph Ngelenge kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya bhangi kilo 168.

Watuhumiwa hao walikamatwa Januari 21 katika stendi kuu ya mabasi jijini Mbeya wakiwa kwenye bajaji, huku dawa hizo zikiwa zimepakiwa kwenye mabegi nane wakitaka kuzisafirisha kwenda mkoani Arusha.

"Watuhumiwa wameeleza kuingiza nchini dawa hizo kutoka nchi jirani na walitaka kuzisafirisha kwa njia ya basi kuelekea Arusha, upelelezi unakamilishwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa," imeeleza taarifa ya polisi.

Tags: chaChamaMbeyaMwenyekitiPolisiSababusiasavijijiniyamshikiliayataja
TNC

TNC

Next Post

No-show in Tanzania: Learning from a missed opportunity

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company