Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Askari wa zimamoto na raia wawili washtakiwa kusafirisha bangi mahakamani

by TNC
January 22, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Askari wa Zimamoto Afikishwa Mahakamani kwa Shtaka la Kusafirisha Bangi

Dar es Salaam – Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Koplo Erick Ndagwa (32), amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilo 193.66.

Ndagwa ambaye ni mkazi wa Kihonda mkoani Morogoro pamoja na washtakiwa wawili wengine, wamefikishwa Mahakamani leo Alhamisi, Januari 22, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 1375 ya mwaka 2026.

Washtakiwa wengine ni Paul Blas, mkazi wa Mbezi Malamba Mawili na Tido Mkude (35) mkazi wa Mwakasege Kinyerezi.

Washtakiwa wamesomewa shtaka lao na wakili wa Serikali, Monica Matwe, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube.

Wakili Matwe alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Desemba 6, 2025 katika Mtaa wa Masoka Kinyerezi wilaya ya Ilala, walikutwa wanasafirisha bangi zenye uzito wa kilo 193.66.

Baada ya kusomewa shtaka lao, Hakimu Makube aliwaeleza washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Pia kiasi cha dawa walichokamatwa nacho haina dhamana.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika, hivyo waliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu Makube aliahirisha kesi hadi Februari 4, 2026 kwa kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na sababu alizozieleza.

Tags: askaribangikusafirishamahakamaniRaiaWashtakiwaWawiliZimamoto
TNC

TNC

Next Post

Regional framework unveiled to boost pandemic preparedness for partner states

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company