Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Familia yalia na gharama za matibabu ya mtoto aliyejeruhiwa na mbwa Iringa

by TNC
January 20, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Familia ya Mtoto Aliyeshambuliwa na Mbwa Iringa Yaomba Msaada

Iringa. Familia ya mtoto Rahmatullahi Ng’amilo (9) aliyeshambuliwa na kujeruhiwa na mbwa wazururaji katika Mtaa wa Don Bosco A, Manispaa ya Iringa imesema inaendelea kupitia kipindi kigumu cha maisha, ikikabiliwa na maumivu ya kihisia na mzigo wa gharama za matibabu.

Wazazi wa mtoto huyo wamesema kuwa maisha ya familia yamebadilika baada ya tukio hilo, wakijikuta wakiishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa kuhusu afya na mustakabali wa mtoto wao.

Baba wa mtoto huyo, Said Ng’amilo amesema tangu tukio hilo kutokea familia imeingia kwenye mzigo mkubwa wa kifedha kutokana na gharama za matibabu.

Gharama za Matibabu Zaidi ya Sh 950,000

Ng’amilo amesema hadi sasa familia imetumia jumla ya Sh 950,000 kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao, fedha ambazo zimekuwa juu ya uwezo wao wa kifedha.

Amesema kati ya fedha hizo, Sh 350,000 zilitumika kulipia huduma ya dharura hospitalini mara baada ya mtoto kufikishwa hospitali, huku Sh 400,000 zikitumika kwa ajili ya huduma ya upasuaji.

"Licha ya mtoto kuwa na bima ya CHF, bima hiyo haigharamii dawa zote, hali iliyotulazimu familia kutumia Sh 200,000 za ziada kununua dawa muhimu kwa ajili ya kuendelea na matibabu," amesema Ng’amilo.

"Mzigo wa gharama hizo umekuwa mkubwa kwa familia, na tunalazimika kuacha shughuli za kujipatia kipato ili kumhudumia mtoto hospitalini, jambo linalozidi kudhoofisha hali ya kiuchumi," ameongeza.

Pia, Ng’amilo amesema hadi sasa familia haijapata msaada wowote kutoka serikalini, hali iliyoongeza maumivu ya gharama katika kipindi hiki kigumu.

Msaada wa Wananchi

Katika hatua nyingine Ng’amilo amesema kuwa msaada pekee walioupata umetolewa na wanamtaa wa Don Bosco A, ambao walichangisha na kutoa Sh 32,000 ili kusaidia kugharamia sehemu ya matibabu ya mtoto huyo.

Kwa sasa, familia ya mtoto huyo inaomba msaada kutoka kwa wadau na jamii kwa ujumla ili kusaidia gharama za matibabu, sambamba na kuitaka serikali na mamlaka husika kuchukua hatua madhubuti kudhibiti mbwa wazururaji ili kuzuia madhara zaidi kwa watoto wengine.

Hali ya Matibabu

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk Alfred Mwakalebela, amesema mtoto huyo alipokelewa Januari 8, 2026 kupitia idara ya dharura kwa ajili ya matibabu ya haraka na baada ya kupokelewa, ilibainika kuwa mbwa hao walimsababishia mtoto huyo majeraha makubwa kichwani na kwenye mapaja ya ndani, huku akiwa anatokwa na damu nyingi.

"Mtoto huyo alihudumiwa haraka, akapatiwa chanjo ya tetenasi pamoja na chanjo ya kichaa cha mbwa ili kuzuia maambukizi hatarishi," amesema Dk Mwakalebela.

Baada ya huduma za awali, Dk Mwakalebela amesema mtoto huyo alilazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kufanyiwa upasuaji katika chumba cha upasuaji (theatre) na baadaye kuhamishiwa wodini.

Aidha kwa sasa, Dk Mwakalebela amesema mtoto huyo anaendelea na matibabu katika wodi namba 6 ya watoto, huku hali yake ikiendelea vizuri na kufuatiliwa kwa karibu na wataalamu wa afya.

Ongezeko la Kesi za Kichaa cha Mbwa

Akizungumzia mwenendo wa matukio kama hayo, Dk Mwakalebela amesema hospitali hiyo hupokea kesi chache za majeruhi wa mashambulizi ya mbwa, lakini mara nyingi hupokea wagonjwa wanaogua kichaa cha mbwa na baadaye hufariki kwasababu wengi wao wakipatwa na majeraha huchelewa kwenda hospitali kupata huduma.

"Kwa mwaka jana hapa hospitali tulipokea kati ya wagonjwa 4 hadi 6 waliogundulika kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa na kufariki," amesema Dk Mwakalebela.

Rahmatullahi alipatwa na majeraha makubwa baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa na mbwa wazururaji 4 mtaa wa Don Bosco A, Manispaa ya Iringa, wakati akiwa njiani kwenda shule ya msingi Nyumbatatu tukio ambalo limeibua hofu miongoni mwa wakazi na kuonesha changamoto ya kudhibiti wanyama hao katika maeneo ya makazi.

Tags: aliyejeruhiwafamiliaGharamaIringaMatibabumbwamtotoyalia
TNC

TNC

Next Post

Youth invited to apply for 2026 service programme

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company