Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Anayedaiwa kujinyonga mahabusu kuzikwa leo akiacha maswali 10 tata

by TNC
January 17, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Maswali 10 Yasiyojibiwa Kuhusu Kifo cha Kijana Moshi

Moshi – Familia ya Michael Rambau (19) inasema maswali mengi hayajapata majibu kuhusu kifo cha kijana wao, wakati maziko yake yakifanyika leo, Jumamosi, Januari 17, 2026. Polisi wanadai alijiua kwa kujinyonga akiwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi mjini Moshi.

Kijana huyo ambaye ni fundi bomba na dereva bodaboda mkazi wa mtaa wa Karikacha, kata ya Rau, mkoani Kilimanjaro anadaiwa kujinyonga kwa kutumia mkanda akiwa mahabusu alikokuwa akishikiliwa Januari 13, 2026 kwa tuhuma za kumjeruhi baba yake mdogo kwa kumpiga bapa la panga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema mtuhumiwa huyo pia alikuwa anatuhumiwa kumuua baba yake mzazi Novemba 22, 2025 kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kisha kutoroka hadi alipokamatwa Januari 13, kwa tuhuma za kumshambulia na kumdhuru baba yake mdogo, Brian Felix.

Msemaji wa familia, Today Rambau, alisema kijana huyo alitofautiana na baba yake mdogo alipochukua spana za gari la marehemu baba yake, aliyefariki Novemba 22, mwaka jana.

"Michael alikamatwa Januari 13, kwa tukio la kumshambulia baba yake mdogo kwa kumpiga na bapa na kupelekwa kituo cha polisi," alisema msemaji wa familia.

"Hili tukio ni tukio la mshituko sana kwa sababu mtu amechukuliwa leo (Januari 13) halafu unapewa taarifa eti kajiua ndani ya mahabusu, hili sio jambo la kufurahisha hata kidogo," alisema baba mdogo wa marehemu.

Familia hiyo pia ilikana kufahamu tuhuma za kijana huyo kumuua baba yake na kuwa alikuwa ametoroka, suala ambalo linaongeza maswali juu ya tukio hilo.

Maswali Yanayoibuka:

  1. Polisi wanasema Michael alijiua kwa kutumia mkanda, je, ilikuwaje akaingia mahabusu na mkanda wakati washukiwa huamriwa kuuvua pamoja na viatu akingali kaunta?

  2. Ilikuwa mshukiwa akapokewa na kuwekwa mahabusu bila kufanyiwa upekuzi kama inavyofanyika kwa wengine?

  3. Kwenye mahabusu aliyowekwa alikuwa peke yake au alichanganywa na mahabusu wenzake?

  4. Kama alikuwa amechanganywa na mahabusu wenzake, ilikuwaje wasimzuie mwenzao kujinyonga au hata kuwajulisha askari?

  5. Kama alikuwa chumba cha peke yake, kwa nini aliwekwa peke yake wakati kosa alilokamatwa nalo lilikuwa la kujeruhi, ambalo kimsingi lina dhamana?

  6. Kama mahabusu wenzake hawakusikia wala kumuona mwenzao akijinyonga, polisi waligunduaje kuna mahabusu amejinyonga na ni wakati gani waligundua?

  7. Kujinyonga kunaendana na purukushani, ilikuwaje kijana huyo akajinyonga bila kusikika purukushani ambazo zingewashtua polisi?

  8. Mahabusu ya kituo hicho na kaunta ya polisi hauzidi umbali wa meta 10 au 20, inawezekanaje mtu ajinyonge bila polisi kusikia purukushani hizo?

  9. Kwa nini mazingira ya kujinyonga mbona hayajafafanuliwa na uchunguzi umefikia wapi?

  10. Polisi wanasema alichukuliwa na kuhojiwa, alihojiwa wapi, kwa muda gani na alirudishwa mahabusu muda gani?
Tags: akiachaAnayedaiwakujinyongakuzikwaleoMahabusuMaswalitata
TNC

TNC

Next Post

Nyavu zinazotelekezwa ziwani tishio

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company