Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwili wa dereva bodaboda wakutwa juu ya kaburi Tabora

by TNC
January 14, 2026
in Swahili
0
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mwili wa Dereva Bodaboda Unafikwa Juu ya Kaburi Tabora

Tabora – Mwili wa Hamisi Nchambi maarufu Ngosha ambaye ni dereva bodaboda umekutwa juu ya kaburi katika makaburi ya Miemba, kata ya Malolo, Manispaa ya Tabora.

Inadaiwa watu wasiojulikana wametelekeza mwili wa kijana huyo ambapo pikipiki yake haikukutwa eneo la tukio.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano, Januari 14, 2026, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Costantine Mbogambi amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa matukio hayo huku likiwasaka usiku na mchana wote wanaohusika na matukio hayo na kuwatia nguvuni.

"Tunaendelea kuwasaka watu hawa na watatiwa nguvuni ili sheria ichukue mkondo wake kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuishi," amesema Mbogambi.

Tukio hilo ni la pili la aina hiyo kutokea ndani ya Januari hii ambapo la kwanza lilitokea kata ya Tumbi wiki moja iliyopita.

Shuhuda wa tukio hilo, Rashidi Mrisho amesema alipigiwa simu na mama yake kuwa kijana huyo amefariki makaburini lakini mikono yake imefungwa kwa nyuma na pikipiki haipo.

Amesema bodaboda huyo ni kijana mwaminifu na ndio wakati wote amekuwa akiagizwa kubeba abiria na bidhaa muhimu za nyumbani, na kazi zote hizo amekuwa akizifanya kwa uaminifu.

"Kwa leo hatujui cha kusema kwa sababu tumekuwa tukisikia tu kwamba kuna mtu kauawa, tulikuwa tukishituka lakini tunachukulia tu ile kawaida lakini leo ameuawa huyu mtu wetu kabisa tumeumia sana," amesema Mrisho.

Hamisi Saidi jirani wa marehemu Hamisi, amesema wamepokea taarifa kuwa Ngosha amefariki dunia kwa kuuawa jambo ambalo limewashangaza kwa sababu anafahamika sio mtu mkorofi.

"Sasa labda hiyo pikipiki mpya ndio sababu."

"Tunahisia tu kwamba labda ameuawa kwa sababu ya hiyo pikipiki kwa kuwa ni mpya, maana kwa uzoefu wetu ukiona bodaboda ameuawa na pikipiki imechukuliwa ujue ni mpya tu, inaumiza sana kutoa uhai wa mtu kwa sababu ya kitu kinachoweza kununulika," amesema.

Aidha Katibu wa bodaboda mkoani humo, Dotto Mwamtuya amelaani tukio hilo huku akiiomba Serikali kuangalia kwa karibu matukio kama hayo kwani kazi ya bodaboda ni moja ya ajira za vijana hivyo yakiwa yanatokea matukio kama hayo wataogopa kufanya kazi.

"Vijana wamejiajiri kupitia kazi hii na wanapata kipato, wanaendesha familia zao lakini sasa wataanza kuogopa ikiwa hali ndiyo hii, maana yule wa Tumbi alifungwa hivihivi kama huyu na akauawa sasa Serikali kwa kweli ituangalie," amesema.

Tags: BodabodaDerevajuukaburimwiliTaborawakutwa
TNC

TNC

Next Post

Teen accused of assault hangs himself while in police custody

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company